Kipofu aanza kuona mara baada ya kusikiliza wimbo wa Dhihirisha
Nivigumu kuamini lakini ukweli ni huo kwamba, mtoto mmoja wa miaka 10, Anna Msingwa aliyezaliwa akiwa kipofu ameanza kuona huku Iringa, kwa mara ya kwanza baada ya wazazi wake kuusikiliza kwa kumanisha wimbo wa Dhihirisha wakiwa na mtoto wao ghafla nguvu ya mungu ilishuka na kujikuta wamezama katika maombi ya kumsihi Mungu amfungue macho kijana huyo, na walipomaliza kuomba mtoto wao walimuona anawaangali na kuanza kushangilia uponyaji.
Akiongea kwa njia ya simu na mratibu wa usambazaji wa albamu ya muziki wa injili ya Ushindi ya mwimbaji Kabula J.George, George Kayala kutokana Iringa, baba mzazi wa mtoto huyo, John Msingwa alisema kuwa, waliamua kuutumia wimbo huo kwa kumanisha kama muongozo wa maombi yao, baada ya kuusikiliza kwa muda mrefu na kubaini kwamba unanguvu zisizo za kawaida, waliamua kuweka wembo huo na kuanza kuabudu nao na walichokitarajia kikawa, na sasa mtoto wao anaona kama kawaida.
“Namshukuru Mungu kwa muujiza huu ambao amenifanyia kupitia wimbo huu, ni vigumu kaumini lakini ukweli unabaki palepale kwamba, mwanangu alikua haoni tangu kuzaliwa, tulipousikia wimbo wa Dhihirisha mimi na mke wangu tulimsihi Mungu ajidhihirishe kwa mwanetu aone kama wengine, na sasa anaona baada ya kuuimba kwa kumanisha wimbo huo,” alisema Msingwa.
Albamu hiyo inapatikana maduka yote ya kanda na kwa wamachinga nchini nzima, na kwa wale watakaoihitaji wawasiliane na mratibu wa idara ya usambazaji kwa namba 0755 240 136.
Post a Comment