LULU, PACHA WA DOTNATA NDANI YA MBEYA AGOSTI 4,2013

WASANII WA FILAMU NCHINI ELIZABETH MICHAEL (LULU) NA PACHA WA DOTNA NI MIONGONI MWA WAGENI WATAKAOHUDHURIA TAMASHA LA KUITAMBULIA ALBAM YA NITANG’ARA TU YA MWINJILISTI KABULA GEORGE UTAKAOFANYIKA KATIKA MKOA WA MBEYA TAREHE 4 MWEZI WA 8, 2013. SEHEMU AMBAPO LITAFANYIKA TAMASHA HILO ITATANGAZWA HIVI KARIBUNI. WASILIANA NASI KWA SIMU NAMBA 0755 240136/0712001880.

JIPATIE SOFA SAFI KWA KOMBA SOFA SHOORM MKOANI MBEYA

KOMBA SOFA SHOORM (YESU NDIYE) NI WATENGENEZAJI WA SOFA ZA KISASA NA KUZIUZA KWA GHARA NAFUU SANA. WAPO MBEYA STRIRED JIRANI NA KANISA LA HIJA MWANJELWA JIRANI NA KANISA KUBWA WA ROMA. WASILIANA NAO KWA SIMU NAMBA 0754553467 AU 0655 553467. NYOTE MNAKARIBISHWA.

ECK PRODUCTION STUDIO YA KISASA NA KIMBILIO LA WAIMBAJI WA MUZIKI WA INJILI TANZANIA.



IPO MWEMBECHAI JIJINI DAR ES SALAAM, TANZANIA WAIMBAJI KAMA ROSE MUHANDO, HABATI BUKUKU, BONY MWAITEGE,UPENDO NKONE, JANGALA SON, MWANSASU NA WENGINE WENGI WAMEREKODIA KATIKA STUDIO HIYO. WASILIANA NAO KWA NAMBA +255 656 388 404

REDIO USHINDI FM KIPENZI CHA WATU WENGI NYANDA ZA JUU KUSINI

MWAMPULULE: Mtandao wa biashara umeharibu huduma ya uimbaji




Leo ni siku ya nane ya mwezi huu wa kwanza na kwenye safu hii tunaye  muimbaji wa muziki wa Injili nchini anayekwenda kwa jina la Emmanuel Mwampulule mzaliwa wa Mbeya lakini sasa masikani yake yapo jijini Dar es Salaam.
Baada ya kukutana na muimbaji huyo mwenye nyimbo zenye mguso wa ajabu, alionekana kuwa na uchungu juu ya waimbaji wa muziki huyo ambao wameugeuza muziki huo kuwa biashara ya kuwaingizia kipato cha kila siku na kusahau wito walioitiwa na Mungu wao.
Mwampulule anasema kuwa, kitendo cha baadhi ya waimbaji kuhitaji kiasi kikubwa cha fedha kwa ajili ya kwenda kuhudumia katika mikutano ya dini, semina, makongamano na makanisani kumeonesha wazi kwamba, watumishi hao wa Mungu wamekuwa wafanya biashara  licha ya kupinga mara kwa mara kauli hiyo ambayo imekuwa ikitolewa na wadau wa muziki huo hapa nchini.
Muimbaji huyo anayeabudu katika kanisa la Mito ya Baraka jijini Dar es Salaam alisema kuwa, waimbaji hasa wenye majina makubwa, baada ya kuinuliwa ili wamtumikie vema Mungu wao kwa njia ya uimbaji na kuwarejesha kundini kondoo waliopotea, wamekuwa wakijiona wao ni bora kuliko wengine na ndiyo maana wamekuwa wakiomba dau kubwa pindi wanapoitwa kwenda kuimba sehemu walikoalikwa.
“Sikatai kwamba, mtumishi anastahili kula kutoka madhabahuni kwake, lakini isiwe kama hawa wenzetu wanavyofanya pindi wakialikwa kwenda kutoa huduma ya uimbaji sehemu, ambapo  hudai pesa nyingi bila kuangalia kwamba kuinuliwa kwake na Mungu ni njia mojawapo ya kuwarejesha kundini kondoo waliopotea kwa njia ya uimbaji.”
Aliendelea kusema kuwa, muimbaji aliyeinuliwa na Mungu na jina lake kuvuma kila pembe ya nchi na hata duniani kwa ujumla, pindi anapoenda sehemu kuimba, watu wengi hukusanyika kwa ajili ya  kumuangalia jinsi anavyoimba na baadhi yao kuamua kuachana na matendo maovu na kuokoka.  Lakini kama ukishindwa kwenda sehemu alikoalikwa, ni dhahiri kwamba watu hao watabaki kama walivyo.
Kana kwamba hiyo haitoshi, Mwampulule alisema kuwa, kitendo cha soko la muziki wa Injili kuonekana kuwa juu kuliko miziki mingine kwa sasa, kumepelekea waimbaji kuinua mabega na kuona kuwa, muda huu ndiyo wa wao kufaidika na upepo huo ambao haujulikani unaweza kuchukua kipindi gani.
Mwampulule aliendelea kudokeza kuwa, waimbaji wote ambao Mungu amewainua na majina yao kufahamika kwa kila rika, watambue kwamba, yeye aliyewainua ana uwezo wa kuwashusha pia akainua wengine ambao watatumika katika roho na kweli bila kuangalia maslahi.
Mtumishi huyo wa Mungu tayari ana albamu yake mkononi aliyoipa jina la Maisha Bila Yesu Utaishije? yenye vibao tisa ambavyo ni Amani utaipata wapi, Amen Haleluya, Kiburi cha uzima, Nani kama Yesu, Akabhalilo (wa kilugha) wenye maana ya Nyakati, Neema na Baraka, Mito ya baraka na Maisha Bila Yesu Utaishije? ambao umebeba albamu hiyo.
Huduma ya uimbaji aliianza mwaka 1998 akiwa kama mwalimu wa  kwaya ya Yerusalemu ya mkoani Mbeya, iliyokuwa chini ya kanisa la Pentekoste. Mwaka 2000 alianza rasmi zoezi la kurekodi albamu yake binafsi na ilikamilika mwaka 2004 na kuiita Maisha Bila Yesu Utaishije?
Mwimbaji huyo ambaye kwa sasa yupo katika mchakato ya kufyatua albamu  ya pili, alimaliza kwa kuwataka waimbaji wa muziki wa Injili kuachana na tabia ya kuendekeza suala la pesa pindi wanapoalikwa kwenda kutoa huduma kwenye makanisa na mikutano ya dini ama kazi zinazohusiana na mambo ya kiroho. Bali watu watakaowaalika nao watakuwa wanatambua kuwa ni kiasi gani ambacho wangependa kuwalipa watumishi hao ili kuendelea na shughuli zao za kihuduma.
Nakukumbusha pia kuwa albamu ya muziki wa Injili  inayokwenda kwa jina la Ushindi ya Kabula J.George sasa ipo madukani nchi nzima. Albamu hiyo imefanyika baraka kubwa kwa watu wenye matatizo mbalimbali na waliofungwa na nguvu za giza, na sasa wako huru wakimtukuza Mungu. Kwa wanunuaji wa jumla na rejareja wasiliana na msambazaji kwa simu namba 0713328290.



Newer Post Older Post