LULU, PACHA WA DOTNATA NDANI YA MBEYA AGOSTI 4,2013

WASANII WA FILAMU NCHINI ELIZABETH MICHAEL (LULU) NA PACHA WA DOTNA NI MIONGONI MWA WAGENI WATAKAOHUDHURIA TAMASHA LA KUITAMBULIA ALBAM YA NITANG’ARA TU YA MWINJILISTI KABULA GEORGE UTAKAOFANYIKA KATIKA MKOA WA MBEYA TAREHE 4 MWEZI WA 8, 2013. SEHEMU AMBAPO LITAFANYIKA TAMASHA HILO ITATANGAZWA HIVI KARIBUNI. WASILIANA NASI KWA SIMU NAMBA 0755 240136/0712001880.

JIPATIE SOFA SAFI KWA KOMBA SOFA SHOORM MKOANI MBEYA

KOMBA SOFA SHOORM (YESU NDIYE) NI WATENGENEZAJI WA SOFA ZA KISASA NA KUZIUZA KWA GHARA NAFUU SANA. WAPO MBEYA STRIRED JIRANI NA KANISA LA HIJA MWANJELWA JIRANI NA KANISA KUBWA WA ROMA. WASILIANA NAO KWA SIMU NAMBA 0754553467 AU 0655 553467. NYOTE MNAKARIBISHWA.

ECK PRODUCTION STUDIO YA KISASA NA KIMBILIO LA WAIMBAJI WA MUZIKI WA INJILI TANZANIA.



IPO MWEMBECHAI JIJINI DAR ES SALAAM, TANZANIA WAIMBAJI KAMA ROSE MUHANDO, HABATI BUKUKU, BONY MWAITEGE,UPENDO NKONE, JANGALA SON, MWANSASU NA WENGINE WENGI WAMEREKODIA KATIKA STUDIO HIYO. WASILIANA NAO KWA NAMBA +255 656 388 404

REDIO USHINDI FM KIPENZI CHA WATU WENGI NYANDA ZA JUU KUSINI

Witness Mallya: Tusiimbe kwa kushindana



Ni siku nyingine imempendeza Mungu tukutane katika safu hii ya tukiwa katika Mwaka Mpya wa 2010. Tuna kila sababu za kumrudishia heshima na utukufu Muumba wetu kwa kutuvusha salama mwaka 2009 ambao ulikuwa na majaribu ya hapa na pale, kwani kuna baadhi ya watu walifanikiwa kutimiza malengo waliyojiwekea na wengine kutokana ba sababu tofauti walishindwa kuyatimiza. Hilo lisikutie shaka, pengine mwaka huo haukuwa wako na wewe umepangiwa kufanikiwa mwaka huu.
Kikubwa nasema kuwa, shukuru kwa kila jambo na Mungu atakisikia kilio chako. Ikiwa leo ni siku ya kwanza ya mwezi huu wa kwanza tunaianza safu hii kwa muimbaji Witness Joseph Mallya mzaliwa wa Kilimanjaro lakini sasa masikani yake yapo jijini Dar es Salaam.
Mara baada ya kukutana na mtumishi huyu wa Mungu, swali langu la kwanza nilitaka kujua, ni kwanini leo hii baadhi ya waimbaji wa muziki wa Injili wamekuwa wakiimba kwa mashindano kama wafanyavyo watu wa mataifa? Licha ya uchanga wake katika huduma hii ya kuimbaji wa nyimbo za Injili, Witness alikiri kuwepo kwa hali hiyo na kusema kuwa, kufanya hivyo ni kumkosea Mungu ambaye hapendi neno lake lishindanishwe.
“Tusiimbe kwa kushindana kama wanamuziki wa mataifa, kwani Neno la Mungu huwa halishindanishwi na wala Mola hapendi tufanye hivyo. Nimezunguka kwenye matamasha mengi ya muziki wa Injili hasa kwenye uzinduzi ambapo waimbaji wengi wa muziki huo hualikwa kwa ajili ya kuimba kabla ama baada ya muhusika kupanda jukwaani.
“Kufika kwangu kwenye matamasha hayo nimejifunza mambo mengi sana likiwemo hili la waimbaji kutegeana kupanda jukwaani na baadhi yao huwaambia hata wasema chochote (MC) kuwapanga wa mwisho baada kuimba wengine ili watakapopanda waimbe kwa kujituma na kuwashawishi watu kuwashangilia ili waonekane wameimba vizuri kuliko wengine,” anafafanua muimbaji huyo.
Katika hatua nyingine muimbaji huyo ameeleza kwamba jambo hili limekuwa likijitokeza katika baadhi ya makanisa na kuifanya kazi hiyo kuwa ya ushindani tofauti na ilivyokuwa zamani ambapo watu walikuwa wakiimba kwa ajili ya huduma.
 “Jambo hili lipo pia makanisani hasa kwenye kanisa lenye kwaya zaidi ya moja. Utakuta waimbaji wanapopewa nafasi ya kuimba hucheza stepu kwa kujituma ili waonekane wao ni zaidi ya wenzao, na baada ya ibada hukaa na kuanza kusema wamewafunika wenzao na wao ni wazuri zaidi.
“Hali hiyo mesababisha kuibuka kwa matabaka ya waimbaji makanisani na nje ya makanisa. Bila woga utasikia  muimbaji anasema ooh! wale hawatuwezi, sisi ni zaidi yao, unaona tulivyowafunika, siku nyingine hawatakubali kupanda jukwaa moja na sisi. Hii siyo sawa na huchangia  waimbaji kuogopana jambo ambalo ni kinyume na malengo  ya Injili,” anasema Witness.
Hata hivyo, Witness anafafanua kwamba kitendo cha waimbaji wa Injili kuimba kwa kushindana kumesababisha kutunga nyimbo zisizo na upako wa Mungu ambazo huwa na utamu kama pipi ambayo hupoteza utamu wake kwa muda mfupi.
“Kutokana na hali hiyo,waimbaji wengi wamejikuta wakiimba bila utukufu wa Mungu, bali wao kama wao ndiyo maana nyimbo zao huwa zinaburudisha tu watu ila hazina uponyaji ndani yake,” anasema Witness.
Kadhalika aliongeza kuwa endapo waimbaji hao wangekuwa wanaimba katika Roho na kweli na kumtanguliza Mungu wao kabla ya uimbaji, lisingekuwa jambo la kushangaza kuona watu wanapokea uponyaji pindi wanapokuwa kwenye matamasha ya uzinduzi wa albamu za nyimbo za Injili, ama kwenye makongamano.
Akizungumzia huduma yake, Witness alisema kuwa, kwa sasa yupo studio anamalizia albamu yake yenye nyimbo nane na tayari nyimbo tatu zipo mtaani  kupitia vituo vya redio kote nchini. Albamu hiyo inakwenda kwa jina la Niite Bwana.
Amezitaja baadhi ya nyimbo zilizopo mtaani hivi sasa kuwa ni pamoja na Niite Bwana, Sifa zako zivume na Tunamtazamia nani? Huku akitarajia kutoka na nyimbo nyingine tano siku chache zijazo.
Nyimbo zinazounda albamu hiyo ni pamoja na Mbona unachelewa sana, Niite Bwana, Sifa zako zivume, Usinitenge, Tunamtazamia nani?, Anatupenda, Nitoe Hivi nilivyo na Nakuulize Mungu.
Witness alimaliza kwa kuwataka waimbaji wenzake kuachana na tabia ya kuimba kwa mashindano badala yake waimbe nyimbo zao katika Roho na kweli ili kuwasaidia watu wenye matatizo mbalimbali kwa maana wao ni watumishi kamili wa Mungu, na nyimbo zao zinanafasi kubwa ya kuwaponya watu ama kuibadili jamii kuondokana na tabia chafu kuliko kuimba nyimbo za kusisimua mwili pekee.



Newer Post Older Post