KWA NINI WATU WENGI HAWAJIBIWI MAOMBI YAO?
Apostle George Kayala |
Wapo wanaoomba ili wananikiwe wapate kuwatishia wenzao,
ama kutumia kinyume na mapenzi ya Mungu kile anachoomba. Unaweza kukuta mtu
anasema mimi naomba Mungu anipe pesa kwa ajili ya huduma yake lakini kumbe
moyoni mipango iko tofauti.
Kaka wewe ni miongoni mwa watu ambao wameomba muda mrefu
bika kupata haja ya kile unachoomba soka kitabu hiki. Yakobo 4:3 “Hata mwaomba walahampati
kwa sababu mwaomba vibaya ili mvitumie kwa
tamaa zenu”.
Ili
Mungu akujibu kile unachoomba inakupasa kuomba sawasawa na mapenzi yake na siyo
yako. Kumbu kuwa Mungu ni Roho, hivyo huwezi kumdanganya kwa lolote katika
maombi yako ambayo naweza kuyaita ni ya ubabaishaji.
Katika
kitabu cha 1Yohana 5:14-15 biblia inasema “Na huu ndio ujasiri tulionao kwake, ya kuwa, tukiomba kitu sawasawa na
mapenzi yake, atusikia. 15 Na tukijua kwamba atusikia, tuombacho chote, twajua
kwamba tunazo zile haja tulizomwomba .
Naamini
mpaka hapo utakuwa umejifunza kitu fulani kwa haya machache niliyokweleza. Nitaendelea
na somo hili kesho naomba usikose kulifuatilia kwani ni imani yangu mpaka
mwisho wa somo utakuwa umejifunza kitu na utabadili mwenendo wa maombi yako.
Elewa
kuwa kila unaloomba Mungu anauwezo nalo na haakuna la kumshinda. Mandiko katika
kitabu cha Yeremia 32:27 yanasema “Tazama mimi ni BWANA Mungu wa wote wenye mwili je! Kuna neno gumu lolote nisiloliweza?.Sikiliza msomaji
mpendwa Hakuna jambo gumu la Kumshinda Bwana.
Naitwa Apostle George Kayala
Kwa maoni na ushauri niandikie
kwa barua pepe gmkproduction77@gmail.com
Post a Comment