KWA NINI WATU WENGI HAWAJIBIWI MAOMBI YAO? - 2
Swali
waliotangulia jana na usiku wa kuamkia leo ina maana hawakuwa na malengo? Jibu ni
kwamba nao walikuwa na malengo kama wewe ila hawakujua siku yao ya kufa na
waliamini kabisa kuwa watatimiza malengo yao. Ni maombi yangu malengo yako
uyaweke mkononi mwa Bwana ili akufanikishe hata kama atakuchukua leo utakuwa na
faida ya kuishi naye milele.
Ame,
ngoja tuendelee na somo letu la KWA NINI WATU WENGI HAWAJIBIWI MAOMBI YAO? Jana nilimaliza
kwa kusema kuwa kila unaloomba Mungu anauwezo nalo na haakuna la
kumshinda. Mandiko katika kitabu cha Yeremia 32:27 yanasema “Tazama mimi ni BWANA Mungu wa wote wenye mwili je! Kuna neno gumu lolote nisiloliweza?.
Kumbuka
kuwa Mungu ndiye ampaye kila mtu ampendaye. Swali la kujiuliza ni kweli wewe
hakupendi mpaka asisikie maombi yako? Kitabu cha Danieli 4:25, 34 maandiko yanasema kuwa; "Aliye
juu ndiye anayemiliki katika ufalme wa wanadamu naye humpa yeye amtakaye, awaye
yote . . . mamlaka yake ni mamlaka ya milele, na ufalme wake hudumu toka kizazi
hata kizazi."
Ukitaka
Mungu akujibu kwa haraka maombi yako, hakikisha unapoingia kwenye maombi uwe
umeshajitakasa na kusamehe wale waliokukosea. Lakini wakati mwingine wewe ndiye
unayesababisha Mungu achelewe kujibu maombi yako kwa sababu unaingia kwenye
maombi ukiwa katika chuki na waliokukosea.
Maandiko
yanasema kuwa “Tunajua
ya kuwa Mungu hawasikilizi wenye dhambi, lakini huwasikiliza wote wanaomcha na
kumtii.” Yohana 9:31. Kama utakuwa na kawaida ya kuingia
katika maombi huku ukiwa na fundo la dhambi ya kutowasamehe waliokukosea na
kujitakasa, hakika utaomba na kufunga mpaka unapata vidonda vya tumbo na
hutapata hitaji la moyo wako.
Maandiko
yanaendelea kusema kuwa “Vumilianeni na
kusameheana. Mtu akiwa na lalamiko lo lote dhidi ya mwenzake, sameheaneni kama
vile Bwana alivyowasamehe ninyi. Zaidi ya maadili haya yote jivikeni upendo,
ambao ndio unaofunga kila kitu pamoja katika amani kamilifu,” Wakolosai 3:13-14. Katika maandiko haya Mungu anatoa amri ya kumsamehe kila mmoja. Hii
inamaanisha kwamba kama unataka kusamehewa dhambi zako lazima kusamehe wale
ambao wamekukosea au wametenda dhambi juu yako.
Na kama hiyo haitoshi
Mungu anakutaka usamehe hata kama unakosewa mara kwa mara. Mathew 18: 21-22; Ndipo Petro akamjia
Yesu na kumwuliza, “Bwana, ndugu yangu anikosee mara ngapi nami nimsamehe? Je,
hata mara saba?” Yesu akamjibu, ‘‘Sikuambii
hata mara saba, bali hata saba mara sabini.’’
Kwa leo naishia hapa nakusihi endelea kufuatilia
somo hilo naamini litakusaidia.
Naitwa Apostle George Kayala
Kwa maoni na ushauri niandikie
kwa barua pepe; gmkproduction77@gmail.com
Post a Comment