MJUE MWIMBAJI MAHIRI WA MUZIKI WA INJILI KABULA.J.GEORGE
Kabula alizaliwa tarehe 26 April 1980 katika kijiji cha Kimiza Wilayani Kwimba mkoa wa Mwanza. Mwimbaji huyo ambaye kwa sasa ameliteka jiji la
Alianza huduma ya kuimba akiwa darasa la tatu katika shule ya msingi Kimiza. Wakati huo alikuwa akienda na mama yake kanisani la Roma Kimiza na alikuwa akiimba katika kwaya ya wadogo mpaka alipohamia Morogoro.
Baada ya kumaliza masomo alihamia Dar es Salaam ambapo alifanikiwa kujiunga na kwaya ya Uinjilisti ya KKKT Tabata Kinyerezi hiyo ikiwa ni mwaka 2005. Hata hivyo Kabula hakudumu
Mwaka 2005 Kabula aliamua kuachana na ukapela na kuamua kuolewa. Baada ya kufunga ndoa Kabula alianza kuimba pamoja na mumewe. Akiwa ndani ya ndoa Kabula kwa kushirikiana na mume wake George Kayala aliamua kuifanyia marekebisho albam yake ya Amani kwa kurudia baadhi ya nyimbo na kuongeza nyingine mpya. Nyimbo alizofanyia marekebisho ni Nkomoji ulioimbwa kwa lugha ya Kisukuma wenye maana ya Mkombozi.
Kuna siri kubwa katika uimbaji, ni zaidi ya kusikiliza ala za muziki na sauti nzuri ya muimbaji, Uimbaji unaomgusa Mungu lazima utawagusa na watu pia, watu wataokoka, wataponywa na watagangwa mioyo
Mwimbaji wa muziki wa injili Kabula John George ni mtumishi wa Mungu anayefanya kazi hiyo kupitia kipawa chake alichopewa na Mungu. Tayari amefafanikiwa kutoa albam ya nyimbo za injili inayojulikana kwa jina PESA na inasambaza na Mam Store.
Watu wengi wamezipenda nyimbo zake kutokana na ujumbe mzuri uliomo na radio mbali mbali za kidini zinacheza nyimbo hizo. Radio ambazo kwa sasa zinapinga nyimbo za dada Kabula ni Wapo Radio, Prise Power zote za
Kabula ambaye kwa sasa wanamuita Mama Pesa kutokana na wimbo wake wa PESA aliouimba kwa mahadhi ya zuku anatoa huduma mbalimbali katika makanisa ya mkoa wa Dar es Salaam na yupo tayari kutoa huduma hiyo ndani na nje ya mkoa wa Dar es Salaam ikiwa ni pamoja na nje ya nchi.
Mwimbaji huyo amekuwa akiwagusa watu wengi wanaozisikiliza nyimbo zake hizo na wamekuwa wakimwalika katika mikutano mbalimbali kwa ajili ya kutoa huduma hiyo ya kuhubiri neno la Mungu kwa njia ya Uimbaji.
Dada Kabula anawakaribisha watumishi wote wa Mungu kumwalika katika semina, mikutano, makongamano n.k kwa ajili ya kulitangaza neno la Mungu wetu kupitia huduma hiyo ya uimbaji.
Nyimbo zilizo katika albam hiyo ni:-
1. Milele
2. Pesa
3. Ninamjua
4. Nkomoji (wimbo wa Kisumuma)
5.
6. Tunakulilia
7. Yatima
8. Nakupa utuku na
9. Niguse.
Kabula anaabudu katika kanisa la Glory Temple Tabata kwa mchungaji James Mwaipyana jijini
Kwa mawasiliano zaidi mpigie simu no:- 0757- 140 336 au 0755 – 240 136
Ama kwa njia ya Email- kabulageorge@yahoo.com
Yupo tayari kufanya nawe huduma mahala popote pale kwa lengo la kumtangaza Mungu.
Post a Comment