PATA HABARI ZA SAKATA LA OIC.
NITAKUWA NAKULETEA SAKATA HILI KUPTIA BLOG HII HABARI AMBAZO ZITAKUWA ZINARIPOTIWA NA VYOMBO VYA HABARI HAPA NCHINI.
Maaskofu waitisha serikali
na Sauli Giliard, Tanzania Daima Okt 24.2008
MAASKOFU wanaounda Jumuiya ya Kikristo Tanzania (CCT), wameeleza kusikitishwa, kushtushwa na kupinga ushawishi unaojengwa na serikali wa kutaka Tanzania iridhie kuanzishwa kwa Mahakama ya Kadhi na kujiunga na Jumuiya ya Kimataifa ya Kiislamu (OIC).
Tamko hilo la kwanza na la aina yake la CCT lilitolewa jana mbele ya waandishi wa habari katika ukumbi wa mikutano wa Luther House jijini Dar es Salaam na kusomwa na Askofu Peter Kitula ambaye ni Makamu Mwenyekiti wa jumuiya hiyo.
Maaskofu hao katika tamko hilo walifikia hatua ya kutoa onyo la wazi kwa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na serikali yake kuhusu kuendelea kukumbatia mjadala wa kuanzishwa kwa mambo hayo mawili.
CCT inayoundwa na makanisa ya Kilutheri, Anglikana, African Inland Church (AIC) na Moravian, ilifikia hatua ya kutoa onyo kwa CCM na serikali yake kuachana na mjadala wa OIC na Mahakama ya Kadhi bungeni na badala yake kuliacha Bunge lijadili masuala mengine muhimu yanayogusa masilahi ya taifa na si yale yenye mwelekeo fulani wa dini.
Tamko hilo liliendelea kueleza kwamba, hawatakuwa tayari kukubalia kwa vyovyote vile kuona chama fulani cha siasa kikijaribu kutafuta ridhaa ya wapiga kura kwa gharama ya kutishia umoja wa kitaifa na amani ya nchi.
“Hapa ieleweke kuwa ni hatari na kamwe isiruhusiwe njia hii kutumika ili mradi chama fulani kishike dola hata kama ni kwa gharama ya kuvunjika kwa umoja wa kitaifa na amani ya nchi hii! Jambo hili hatutalikubali kwa vyovyote vile kwa chama chochote kitakachokubali mambo haya mawili aidha wakati wa kampeni za uchaguzi au wakati wowote ule,” lilisema tamko hilo la CCT lililoambatanishwa na majina ya maaskofu 64 wa nchi nzima.
Pasipo kufafafanua huku wakisema kwamba CCT, haifungamani na chama chochote cha siasa, maaskofu hao katika tamko lao walisema, iwapo itafikia hatua ya Tanzania kujiunga na OIC na Mahakama ya Kadhi kuridhiwa, basi wao watalazimika kufikiria upya jinsi ya kukishauri chama hicho tawala kwa kuzingatia kile walichokieleza kuwa ni manufaa ya Watanzania.
“Japo Jumuiya ya Kikristo Tanzania haifungamani kwa namna yoyote ile na chama chochote cha siasa, haya yakitokea itabidi tufikirie upya jinsi ya kukishauri chama hicho kwa manufaa ya Watanzania wote!” lilisema tamko hilo, ambalo linaonyesha dhahiri kuwa ni onyo la wazi la kukaribia kukataa kukiunga mkono chama hicho tawala na kisha likaendelea:
“Kipekee wakati huu, kutokana na yanayoendelea kujadiliwa bungeni, tunatoa tahadhari kwa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na serikali yake kutoruhusu kabisa kuendelea kwa mjadala huu kama ambavyo tumekuwa tukiomba mara kwa mara kwa nyakati tofauti zilizopita,” linasema tamko hilo. (Pichani ni baadhi ya Maaskofu wa madhehebu mbalimbali nchini wakiwa katika picha ya pamoja na Waziri Mkuu Mh.Pinda mwenye suti nyeusi, picha hii ni kwa hisani ya blog)
Pamoja na hilo, maaskofu hao wamemtaka Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe, kujiuzulu wadhifa wake kutokana na hatua yake ya kujenga ushawishi wenye mwelekeo wa kidini wa kuiingiza nchi katika OIC. Mbali ya hayo, tamko linasema hatua ya Tanzania kujiunga OIC inakwenda kinyume cha Katiba ya Jamhuri ya Muungano, Ibara ya 19 (2) na Sheria ya Vyama vya Siasa nchini.
Askofu Kitula alisema, wanapinga Tanzania kujiunga na OIC kwa maelezo kuwa, katiba ya jumuiya hiyo imejipambanua wazi kuwa na malengo ya kuendelea na kuulinda Uislamu, jambo ambalo ni hatari kwa usalama wa taifa, lenye watu wa imani nyingine za dini.
“Msimamo wetu kuhusu mambo haya mawili ni kuyakataa kabisa na mamlaka yoyote ya nchi kuendelea kukaribisha mjadala huu ili hatimaye ukubalike, ni kupoteza muda wa wenye dhamana ya mamlaka ya nchi hii na rasilimali zake,” linasema tamko hilo.
Akifafanua askofu huyo alisema, katika Ibara ya 1 (11) ya Katiba ya OIC, kuna kipengele kinachosomeka ‘kusambaza, kuendeleza na kuhifadhi mafundisho ya dini ya Kiislamu….kuendeleza utamaduni wa Kiislamu na kuulinda urithi wake’, maelezo ambayo ni kinyume cha Katiba ya Jamhuri ambayo inahimiza uhiari na uhuru wa mtu binafsi katika masuala yanayohusu kueneza dini au masuala ya imani.
Askofu Kitula ambaye alisoma tamko hilo kwa niaba ya Mwenyekiti wa CCT, Akofu Donald Mtetemela, aliyesaini tamko hilo, alisema uamuzi wa kujiingiza katika masuala ya namna hiyo ni wa hatari, kwani yanaweza kuleta migogoro kutokana na kuwapo kwa dhana ya udini.
“Tuna uhakika kuwa yaliyomo katika taasisi ya OIC ni hatari kabisa kwani ikiruhusiwa, katiba ya nchi itakuwa imevunjwa na Watanzania wataingizwa katika migogoro itakayoua maridhiano, mshikamano, amani, utangamano na umoja wa kitaifa,” ilisema sehemu nyingine ya tamko hilo kali na la aina yake kutolewa na taasisi yenye nguvu kidini.
Hofu hii ya CCT kwa mujibu wa tamko lao, inachangiwa zaidi na jinsi ambavyo wabunge na viongozi wa kisiasa walivyojiingiza kujadili mambo hayo mawili, huku wakijua yana masilahi ya kidini zaidi ya utaifa na huku wakielewa wazi ni kukiuka katiba.
“Sisi viongozi wa CCT kwa kuzingatia wajibu wetu wa kinabii na kitume, tunatoa wito kwa Bunge letu lisikubali kamwe kuanzishwa kwa Mahakama ya Kadhi …wala kuridhia uanachama wa Tanzania katika IOC,” lilisema tamko hilo na kwamba amani ya Tanzania imetokana na tunda la dini, itikadi, makabila, rangi na jinsia zote.
Akizungumza katika mkutano huo wa jana na wanahabari, Askofu Dk. Owdenburg Mdegela, alipinga mifano inayotolewa na Waziri Membe kwa nchi zilizokwisha kujiunga na OIC na kudai kuwa mifano hiyo ni sawa na kujifananisha na mtu aliyeshindwa na kuongeza kwamba, waziri anayetoa msukumo wa Tanzania kujiunga na jumuiya hiyo, anapaswa kujiuzulu.
Askofu huyo alimtaka Waziri Membe kuachana na kauli zake juu ya umuhimu wa kuingia kwenye jumuiya hiyo ya Kiislamu na kuhoji aliyemtuma kufanya hivyo.
“Membe aache hizo kauli, kauli zenyewe ni za mitaani…tunampa kadi nyekundu…kwanza ni nani kamtuma, atueleze, iwapo ni Baraza la Mawaziri, Bunge,” alisema na kumtaka ajiuzulu ili kuonyesha ukomavu wa kisiasa.
Alisema kuanzia leo (jana), hawatanyamaza kupinga suala la kujiunga na OIC na kuanzisha Mahakama ya Kadhi na kwamba wataanzisha sala maalumu kwa muda wa mwaka mzima kuhakikisha jambo hili halifanikiwi.
Naye Askofu Dk. Stephen Munga (KKKT), alionyesha wasiwasi na maneno ya Waziri Membe, kuwa hayana utafiti wa kutosha na kuongeza kuwa ni bora kujadili kwanza jinsi ya kuvunja katiba kwa kuwashirikisha Watanzania wote kwani ilivyo, sasa kuunga mkono hoja ya kujiunga na OIC ni sawa na kuikiuka katiba na misingi ya sheria ya nchi.
Naye Askofu Sylivester Gamanywa wa Wapo Ministries aliyeungana na CCT, alisema kuwa, suala la kuijiingiza OIC ni hatari kwani litasababisha umwagaji damu na akamtaka Rais Kikwete kuingilia kati, kunusuru mgawanyiko huu.
Gamanywa alidai waumini wake wamekuwa wakimsumbua juu ya Tanzania kutaka kuanzisha Mahakama ya Kadhi na kujiunga na OIC na kudai kuwa tamko la CCT, ndilo jibu kwa waumini na ndio msimamo wa makanisa mengine yote.
Juzi Waziri Membe ilitoa kauli ya kuwataka Watanzania kuondoa woga juu ya OIC na kudai kuwa kuna nchi zilizojiunga na hazijaathirika kwa namna yoyote na kuongeza kuwa, hakuna nchi iliyo takatifu duniani.
Membe alitoa mfano wa nchi ya Uganda yenye asilimia 10 ya waumini wa dini ya Kiislamu na asilimia 66 ya Wakristo, ambao pamoja na kujiunga na OIC, haina tatizo, hivyo haoni sababu kwa nini Tanzania isijiunge na jumuiya hiyo na kunufaika na fedha za shetani.
Waziri Membe akana kuubeba msalaba OIC
Na Ramadhan Semtawa
WAZIRI wa Mambo Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Bernad Membe, amekuja juu akisema baadhi ya watu wamekuwa wakimtwisha mzigo kwamba, ameingiza Tanzania katika Jumuiya ya nchi za Kiislam Duniani (OIC), kitu ambacho si kweli.
Kauli hiyo ya Membe ni ya kwanza kuitoa hadharani tangu kuibuka kwa kasi kwa mjadala huo, ambao unaonekana kuigawa nchi katika misingi ya kiitikadi.
Akizungumzia hilo jijini Dar es Salaam jana, Membe alisema si kweli kwamba Tanzania imekwishajiunga na OIC na wala yeye hajasema lazima ijiunge.
Membe akifafanua huku akionekana kuguswa na tuhuma hizo dhidi yake kutokana na kutamka hilo bunge katika hotuba ya bajeti ya wizara yake, alisema uamuzi wa kujiunga au la, uko kwa wananchi.
"Nimekuwa kimya, kuachia na kusikiliza watu waseme, jamani, Tanzania haijajiunga na OIC wala sijasema lazima ijiunge," alisema na kuongeza:
"Uamuzi wa kujiunga au kutojiunga utakuwa chini ya wananchi, wasomi, NGOs na ninyi waandishi wa habari, ndiyo mtakaoamua."
Membe alikuwa akifafanua kuhusu uhusiano kati ya Tanzania na Iran, ambao unaonekana na baadhi ya watu kama wenye nia ya kuingiza nchi OIC.
(pichani ni Waziri Membe, picha kwa hisani ya blog)Akifafanua zaidi, alisema watu wasiingize vitu visivyokuwa na msingi kwa ajili ya kutunga na kuzungumzia hisia, na kushauri wasome historia kufahamu uhusiano kati ya nchi hizo mbili.
Membe huku akionekana kuchukizwa na fikra mbovu za kupandikiza udini katika nchi, alisema Watanzania ni watu wanaoheshimika duniani kwa umakini wao, ni aibu na haipendezi kujadili udini.
Alisema kama ni kujiunga na OIC ni jambo la kuamua, kwani Uganda ambako kuna Waislam asilimia 10 imeweza kujiunga huku Wakristo wakiwa ni asilimia 66 na wengine wapagani.
"Sasa jamani, msitake kunichinganisha na watu wangu, nawaambieni tena na tena, Tanzania haijajiunga na OIC na haitaweza kujiunga uamuzi huo ni ridhaa ya wananchi," alisisitiza.
Kwa ufafanuzi, alisema aliwahi kuzungumzia ripoti ya utafiti ya Juni mwaka 1993, ambayo inatoa mapendekezo matatu ambayo ni pamoja na kuingia kuwa kama mwangalizi kisha wananchi wataamua.
Akizungumzia zaidi uhusiano huo na Iran, Membe alisema ziara yake ya hivi karibuni ililenga kuomba kupunguziwa au kufutiwa deni la zaidi ya sh 270 bilioni, ambazo Tanzania inadaiwa.
"Sasa mtu anapohoji urafiki wetu na Iran, ana maana gani, anataka hizi fedha tuzilepeje, kama taifa lina matatizo yake sisi hayatuhusu, tunasimamia maslahi ya taifa," alisema.
Katika hatua nyingine, Membe alionya mwamko wa demokrasi ya mgawanyo wa madaraka baada ya uchaguzi na kwamba, mfumo huo unaojengeka ni wa hatari.
Alisema haiwezekani kuruhusu utaratibu huo kwani utazidi kuhatarisha demokrasi katika bara la Afrika na kuongeza kwamba, ni vema demokrasi ikaheshimika wakati wa uchaguzi.
"Huu mtindo wa baada ya uchaguzi watu kuanza kupiga kelele, sijui siridhiki, kisha wagawane madaraka asilia 40, ni wa hatari, lazima ukomeshwe na usiendelee," alionya Membe.
Hivi karibuni kumeibuka mtindo, ambao chama tawala hugawana madaraka na vyama vingine vya upinzani kama ilivyofanyika baada ya uchaguzi mkuu wa Desemba 27 mwaka jana nchini Kenya, kati ya ODM na PNU na sasa Zimbabwe kati ya ZANU-PF na MDC.
SERIKALI NAYO ILIAMUA KUJIBU

Serikali haijaamua kujiunga OIC
Daily News; Saturday,October 25, 2008
Serikali imefafanua kwamba haijaamua kujiunga na Jumuiya ya Kimataifa ya Nchi za Kiislamu (OIC). Ofisa Mwandamizi wa Serikali aliiambia HabariLeo jana kwamba uamuzi wowote kuhusu suala hilo utawahusisha Watanzania, lakini bado hakuna uamuzi ambao umechukuliwa. Hatua hiyo imekuja baada ya Jumuiya ya Kikristo Tanzania (CCT), kumtaka Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe, ajiuzulu wadhifa wake wa kisiasa iwapo ataendelea kupigia debe suala la Tanzania kujiunga na Jumuiya ya Kimataifa ya Nchi za Kiislamu (OIC). Membe akizungumza juzi na wanahabari alionyesha kushangazwa na hatua ya baadhi ya Watanzania kuogopa Tanzania kujiunga na OIC. Waziri huyo alifafanua kuwa Tanzania haijajiunga na OIC, bali iko kwenye mchakato wa kufanya hivyo. Alifafanua kuwa hata hivyo suala la Tanzania kujiunga ama kutojiunga na OIC liko mikononi mwa Tanzania. Alisema makundi yote ya wananchi watatoa mawazo yao hivyo kwa sasa hakuna haja ya kuogopa wala kuzusha mijadala isiyokuwa na manufaa kwa nchi. “Waziri anayesukuma suala hili, anatakiwa ajiuzulu aache kuzungumzia suala hilo, kwani wananchi wamewatuma kuzungumzia masuala ya OIC?” Alihoji Askofu Dk. Owdenburg Mdegela baada ya kusomwa kwa tamko la maaskofu wa CCT jana Dar es Salaam. Naye Askofu Dk. Steven Munga alisema wao hawasimamii udini, bali wanasimamia Utanzania na akafafanua kuwa baraza hilo linasubiri suala hilo lipelekwe bungeni ndipo na wao watajua cha kufanya. Dk. Munga alisema kitendo cha Membe kutoa mfano wa Uganda kuwa inanufaika na OIC hakina manufaa kwani Watanzania ambao alisisitiza hawana cha kujifunza kwa taifa hilo ambalo alidai limegubikwa na vita ya wenyewe kwa wenyewe kwa muda mrefu. Askofu Sylvester Gamanywa alidai pingamizi la CCT sio la chuki kwa Uislamu ila ni pingamizi la kuzuia mgawanyiko wa kitaifa iwapo taasisi kama OIC itaingizwa kwenye mamlaka ya nchi. Pingamizi hilo lililosainiwa na Mwenyekiti wa CCT Askofu Mkuu Donald Mtetemelwa, walidai endapo nchi itaingia katika OIC, Katiba itakuwa imevunjwa na Watanzania wataingizwa katika migogoro itakayoua maridhiano, mshikamano, amani, utangamano na umoja wa kitaifa.
Post a Comment