ALBAMU YA MNYAMA KOBE YAZINDULIWA
Mtumishi wa Mungu Lukamaja Masunga akiimba wimbo wa kumtukuza Mungu siku ya uzinduzi wa albam yake uliofanyika katika kanisa la TAG Salasala jijini Dar es Salaam. Nyuma ni baadhi ya waimbaji wake nao wakimwimbia Mungu.
Hapa Mtumishi wa Mungu Lulakamaja akimwabudu Mungu wake akiwa na kundi lake. Siku hiyo alikuwa akizundua albamu yake ya kwanza inayokwenda kwa jina la Mnyama Kobe.
Mtumishi wa Mungu Lukamaja Masunga akiimba kwa hisia siku ya uzinduzi wa albamu yake uliofanyika hivi karibuni kwenye kanisa la TAG Salala jijini Dar es Salaam.
Ni mzaliwa wa Shinyanga, alianza kazi ya uimbaji tangu mwaka 1994 akiwa shule ya sekondari Lyamungo-Moshi mkoani Kilimanjaro, kipindi hicho alikuwa akiimba katika vikundi na kwaya za shuleni. Mwaka 1996 alifanikiwa kuwa mwalimu wa kwaya ya International Inland Church lililopo Magadini Moshi. Mwaka 1998-1999 akiwa shuleni, alifanikiwa kuunda kundi la uimbaji alilolipa jina la Comfort Band-Mkwawa High school.
Mwaka 2000, alianza rasmi kuwa muimbaji wa kujitegemea. Akiwa tayari ni muimbaji binafsi mwaka 2002 - 2004 alifanikiwa kuifundisha kwaya ya Kanisa la TAG Madawi-Old Moshi. Mbali na kuwa mwalimu wa kwaya, Lukamaja ameitumika katika maeneo mbalimbali nchini.
Mwaka 2008, alifanikiwa kurekodi albamu yake ya kwanza aliyoipa jina la Mnyama Kobe ambayo inatamba kwa sasa katika vyombo mbalimbali vya habari nchini hasa radio za kidini.
Post a Comment