Misiri kuruhusu waandamanaji 100 kuingia Gaza.
Viongozi wa wanaharakati ambao wamekwama mjini Cairo wamekubali pendekezo la Misiri jana Jumanne kuwaruhusu wanaharakati 100 tu miongoni mwa wanaharakati 1,300 kuingia katika eneo la Gaza lililozingirwa na majeshi ya Israel baada ya wanaharakati hao kufanya maandamano pamoja na mgomo mkubwa wa kula.
Uamuzi huo umewagawa wanaharakati hao kutoka karibu nchi 40 ambao wamekwenda mjini Cairo wakipanga kuingia katika eneo hilo la Wapalestina, ambalo linapakana na Misiri katika eneo la mpakani la Rafah.
Baadhi ya watayarishaji wamesema kuwa pendekezo la Misiri ni ushindi baada ya hapo kabla kukataa kuwaruhusu wanaharakati hao kuingia ukanda wa Gaza kwa ajili ya maandamano yanayoitwa ya uhuru , ambayo yanapangwa kufanyika kesho Alhamis.
Post a Comment