Netanyahu akutana na Rais Hosni Mubarak wa Misri
Cairo:
Waziri Mkuu wa Israel, Benjamini Netanyahu, amekutana na Rais Hosni Mubarak wa Misri mjini Cairo hii leo juu ya juhudi za Marekani za kutaka kuendelea kwa mazungumzo ya amani Mashariki ya Kati yaliyokwama karibu mwaka mmoja sasa.
Hata hivyo, hakuna kiongozi yoyote kati yao aliyezungumza na vyombo vya habari baada mkutano huo, lakini ofisi ya Netanyahu imesema mazungumzo yalikuwa mazito na ya kirafiki.
Ofisi hiyo ilisema viongozi hao walijadiliana namna ya kuanzisha mchakato wa amani na Wapalestina, na juhudi za kumrudisha Gilad Shalit, mwanajeshi wa Israel aliyetekwa na wanamgambo wa Gaza miaka mitatu na nusu iliyopita.
Marekani imekuwa ikiandika barua kwa Israel na Wapelestina ikishadidia kwamba itakuwa mdhamini na kuchukua jukumu la kuanzishwa mazungumzo ambayo mwisho wake yatapelekea kuanzishwa kwa taifa huru la Palestina.
Post a Comment