Urusi kujenga mfumo wa mashambulizi ya makombora
Moscow:
Urusi imesema imedhamiria kujenga mpango wa mfumo wa mashambulizi ya makombora ili kukabiliana na mpango wa Marekani wa kinga dhidi ya makombora.
Waziri Mkuu wa Urusi, Vladmir Putin, alitoa tangazo hilo wakati wa ziara yake katika mji wa Vladivostok uliopo Mashariki ya Mbali ya nchi hiyo.
Mnamo mwezi Septemba, Rais Barack Obama wa Marekani aliufuta mpango wa Marekani ulioanzishwa na mtangulizi wake, George W. Bush, wa kujenga mfumo wa kujikinga dhidi ya makombora kutoka Iran katika nchi za Poland na Jamhuri ya Czech.
Putin alisema mpango wa Marekani wa ujenzi wa mfumo wa kujikinga na makombora ulikuwa ni kikwazo kikubwa katika mpango wa nchi hizo wa kupunguza silaha za nyuklia.

Post a Comment