Eritrea yailaumu Ethiopia kwa kuishambulia
Kwa mujibu wa shirika la habari la AFP, wizara ya mambo ya nje ya Eritrea imesema wanajeshi wa chama tawala cha Ethiopia cha Tigrai People's Liberation Front-TPLF walishambulia eneo la Zalambesa siku ya Ijumaa. Ripoti hiyo pia imesema kuwa maafisa wa Ethiopia hawakupatikana kutoa maelezo yao kuhusu suala hilo .
Chama cha Waziri Mkuu wa Ethiopia , Meles Zenawi cha TPLF ni mwanachama mkuu katika serikali ya muungano na kilikuwa mshirika wa karibu wa serikali ya Eritrea kabla ya nchi hizo mbili hazijaanza kugombania eneo la mpakani.
Post a Comment