Marekani na Uingereza zafunga balozi zao Yemen.
Sana'a:
Marekani na Uingereza zimefunga balozi zake zilizoko katika mji mkuu wa Yemen, Sana'a.
Balozi hizo zimefungwa kutokana na vitisho vinavyotolewa na tawi la Mtandao wa Kigaidi wa Al Qaeda katika rasi ya Arabuni, kushambulia maslahi ya Marekani nchini Yemen.
Baada ya kushindwa kwa jaribio la kulipua ndege ya abiria ya Marekani siku ya Krismas, Waziri Mkuu wa Uingereza Gordon Brown alisema Uingereza na Marekani zinaimarisha juhudi zake za kukabiliana na ugaidi nchini Yemen, nchi ambayo imekuwa kituo cha magaidi wenye msimamo mkali.
Oton Brown
''..Anasema Yemen imetambulika kama Somalia, kuwa eneo moja wapo ambalo sio tu wanapaswa kulitizama, lakini wanapaswa kulichukulia hatua zaidi.
Aidha amefahamisha kuwa ushirikiano katika kukabiliana na ugaidi unaimarishwa zaidi...''
Hatua mbalimbali tayari zimechukuliwa kupambana na ugaidi nchini humo, ikiwemo kulisaidia jeshi la nchi hiyo na kutoa msaada wa kifedha kwa kikosi cha nchi hiyo cha kupambana na ugaidi.
Kamanda wa Marekani katika eneo la Mashariki ya Kati, Jenerali David Petraeus amekutana na Rais wa Yemen Ali Abdullah Saleh kuzungumzia hatua za kuchukua kukabiliana na wapiganaji nchini humo.
Post a Comment