Marekani yatangaza utaratibu mpya kwa wasafiri waingia nchini humo.
Washngton:
Idara inayohusika na Usalama wa Usafari nchini Marekani imetangaza ukaguzi zaidi kwa wasafiri wa ndege kutoka Nigeria, Yemen, Pakistan, Afghanistan, Saudi Arabia na nchi nyingine tisa.
Utaratibu huo mpya wa Usalama, ambao unaanza kutumika leo, utawataka wasafiri kabla ya kupanda katika ndege kukaguliwa mwili mzima, kukagua mizigo, ikiwemo pia kuchunguza vifaa vya milipuko.
Sheria hiyo mpya imekuja kufuatia jaribio la kulipua ndege ya Marekani ilipokuwa ikijiandaa kutua katika Uwanja wa ndege wa Detroit siku ya Krismas, jaribio ambalo lilifanywa na raia wa Nigeria, ambaye Marekani inaamini kuwa amepewa mafunzo na mtandao wa Al Qaeda ulioko Yemen.
Post a Comment