Rompuy atangaza uchumi kuwa mada kuu ya mkutano ujao wa Umoja wa Ulaya.
Rais wa Umoja wa Ulaya Herman Van Rompuy ametangaza kuwa, Uchumi utakuwa mada kuu katika mkutano ujao wa baraza la umoja huo, utakaofanyika Februari 11.
Herman Van Rompuy ambaye ni Rais wa kwanza wa kudumu wa Umoja huo, ameyasema hayo katika siku yake ya kwanza ofisini.
Amesema umoja huo unahitaji kuhakikisha ukuaji wa uchumi barani Ulaya.
Hispania, nchi ambayo tangu januari mosi inashika nafasi ya Urais wa Umoja wa Ulaya, kwa kipindi cha miezi sita, imeeleza pia kuupa kipaumbe uchumi katika kipindi cha uongozi wake kwenye umoja huo unaojumuisha nchi 27 za Ulaya.
Post a Comment