Urusi yaanza kupeleka mafuta Belarus.
Naibu Waziri Mkuu wa Urusi Igor Sechin ametangaza kwamba nchi yake imeanza kupeleka tena mafuta kwenda Belarus , baada ya kusitisha Januari mosi.
Amesema mafuta yalianza kutiririka siku ya Jumapili na kwamba usambazaji katika nchi za Ulaya magharibi haukuathirika.
Urusi na Belarus zimekuwa zikibishana juu ya bei ya mafuta na pia gharama za upitishaji kwa mwaka 2010.
Mabishano hayo yalisababisha kupanda kwa bei ya mafuta kwa zaidi ya dola 80 kwa pipa siku ya Jumatatu.
Post a Comment