Peter Baguma: Aweka Bongo Flava pembeni ili amtumikie Bwana
Alipojitoa kwenye kundi hilo alilodumu nalo kwa miezi nane kabla ya kusambaratika, aliamua kujitosa rasmi kwenye uimbaji wa kujitegemea akiwa na lengo la kuwasaidia watu wa hali ya chini.
Anaeleza kuwa katika albamu yake ya kwanza ambayo inajulikana kwa jina la Yesu Nuru Yangu, aliwashirikisha vijana mbalimbali wanaoishi kwenye mazingira magumu.
“Niliwasaka mitaani na kuimba nao ili kuona wenye vipaji kisha nikawachukua na kufanya nao kazi, walijisikia amani na wengi wameonyeshwa kufurahia tendo hilo ,” anasema Baguma.
Akielezea ugumu anaokutana nao kwenye kazi hiyo ni vitendo vya ‘maprodyuza’ kuweka kipaumbele fedha kuliko kazi, hali inayochangia kuwakatisha tamaa waimbaji walio wengi.
Anafafanua kuwa kuna baadhi ya wadau wameugeuza muziki huo kuwa biashara, hivyo kushindwa kufanya katika ufanisi unaotakiwa kutokana na kuiga vipaji vya watu wengine na kuacha vipaji vyao halisia vikipotea.
Kitu cha msingi kinachotakiwa ni mtu kujitahidi kutoka katika hali halisi aliyo nayo na kujiboresha zaidi kwa kutoiga kwa mtu mwingine ili kuuboresha zaidi muziki wa Injili kuweza kuwa na ladha tofauti zitakazosaidia kuuweka juu siku zote.
“Ili kuuendeleza muziki wa Injili hapa nchini ni vyema waimbaji wanaochipukia wajaribu kuwa wabunifu katika kazi zao na wawe wepesi kujifunza kutoka kwa wanaojua pindi wanapoambiwa kwa ajili ya maboresho na kuwa na msimamo wa hali ya juu katika maamuzi yao.
“Kuna wanamuziki wenye majina makubwa wamekuwa na wivu wa kutotaka kutoa ushirikiano kwa chipukizi kwa kuwapa msaada, ili waweze kufanya vizuri zaidi kitu ambacho kinarudisha nyuma maendeleo ya muziki wa Injili nchini.
“Wivu usio na faida hauwezi kutufikisha mbali ni vema waimbaji wakaondokana na tabia ya ubinafsi katika kumuimbia Mungu ili kuweza kupiga hatua zaidi kwa kutomdharau mtu yeyote na ukweli kwamba wivu unasababisha matatizo kwenye milango ya mbele,” anasema Baguma.
Anamalizia kwa kusema kuwa ili fani yao izidi kupiga hatua, vijana wanaochipukia wasikate tamaa katika kuimba, wajitume ili wasonge mbele na kuangalia kile wanachotaka kufanya kiwe na msukumo wa hali ya juu pamoja na kuwa na imani katika kazi.
Post a Comment