ROSE MUHANDO APASUA NDOA YA MTU
Chanzo cha habari hii kimepasha kuwa, ndoa hiyo ina ‘masiku kibao’ sasa ‘inapumulia mashine’ huku Rose akitajwa tajwa kuhusika na mgogoro wake.
Chanzo hicho kikaendelea kuweka ‘nje’ siri kuwa, chanzo cha kuwepo kwa ufa katika ndoa hiyo ni kufuatia mke wa Msama, Laura kuchezwa na machale kuhusu ukaribu kati ya mumewe na Rose Muhando kiasi cha kukosa amani kama siyo furaha.
Habari zinazidi kumwagika kwamba, hali hiyo ikashamiri, ikanawiri, ikafika mahali hisia za mwanamke huyo zikawa wazi na hivyo kuanza ‘kumsomea’ mashitaka mumewe akitaka maelezo kuhusu ukaribu huo.
Habari zaidi zinapasha kuwa, licha ya kujitetea bila ‘mwanasheria’, bado mke huyo akaweka ngumu kuelewa hali iliyosababisha kila mtu kuanza kuishi kivyake ndani ya nyumba.
“Hii hali ilifika mahali kila mmoja akawa kivyake ndani, Msama akashika hamsini zake, mkewe naye anakumbatia zilizobaki,” kilisema chanzo.
Kikaongeza: “Kubwa kuliko zote, kuna wakati Msama akipiga wimbo wowote wa Rose (Muhando), mkewe anazima redio au anapunguza sauti, moyo unamtuma kuwa, hisia zake zina ukweli.”
Habari zaidi zinasambaa kuwa, hata pale Msama anapokwenda Dodoma kwa shughuli za kikazi, mkewe hudhani ‘mista’ wake yupo ‘andapromisi’ na Rose hali ambayo imekuwa ikizidi kuvuruga ndoa hiyo.
Mambo yalipozidi kuwa mabaya, nyeti zinapasha, mke aliamua kuondoka nyumbani hapo na kwenda ‘kujichimbia’ sehemu moja jijini Dar es Salaam (Risasi linahifadhi jina kwa sasa).
UTETEZI WA WADAIWA
Kufuatia madai haya, blgo hii ilipiga ‘jaramba’ mpaka ofisini kwa Msama, Msama Promotion, Block 41, Kinondoni jijini Dar na na kufanikiwa kuongea naye kwa kumpa ‘a e i o u’ ya ishu yake ambapo alipagawa kwa kuanza kutaka kujua ‘sosi’ wetu.
Alipokataliwa kutunza maadili, alisema mambo ya kifamilia yaachwe kwa wanafamilia, kwani ni jukumu lao kuweka sawa kwenye ‘korogesheni’ endapo mambo yataharibika.
“Mambo ya kifamilia yabaki kuwa hivyo, kama kuna tatizo linalomshirikisha Rose Muhando si kihivyo, hata wewe mkeo anaweza kukuuliza kuhusu mwanamke flani ukamwelewesha, akaelewa na mkaendelea na safari yenu ya maisha,” alisema Msama.
TGM: Kwa hiyo ni kweli?
Msama: Nimeshakupa jibu kaka, mimi kwangu ni amani tu, hakuna wasiwasi wowote ule.
Aidha, TGM ilikachanganya miguu kumsaka Laura, mke wa Msama lakini baadaye akapatika kwa njia ya simu ya kiganjani.
Kwa upande wake baada ya kupigwa ‘mashuti’ na TGM alisema nyumbani kwake hakuna tatizo na wala hana kinyongo na Rose kisha papo hapo akaiomba TGM imtwangie simu baada ya dakika tano, (eti) ana mgeni.
TGM ilizifuata sekunde kwa macho angavu hadi zilipotimu dakika tano, alipopigiwa tena, cha ajabu, akawa anakata simu.
TGM halikuchoka, likamgeukia bingwa wa muziki wa Kwaito, Rose Muhando ambaye kwa ‘binafsi’ yake alisema tuhuma dhidi yake na Alex Msama ni maneno ya ‘wachovu’ wa kiimani, lakini akakiri kuwa karibu sana na Promota huyo kwa sababu za kikazi.
Alipobanwa sana kwamba kuna madai ya malalamiko ya Laura, Rose alisema anaapa kwa Mungu wake kwamba, hakuna ‘malavidavi’ kati yake na Msama na Laura kwake ni wifi yake kwa kuwa Msama kwake ni kama kaka yake ingawa si wa damu moja.
KUMBUKUMBU ZA NYUMA
Mwaka 2007, gazeti moja nchini liliwahi kuripoti kuwepo kwa uhusiano usiofaa kati ya Msama na Rose, wakati huo Promota huyo alikuwa kwenye vikao vya maandilizi ya harusi yake na Laura, lakini wenyewe waliruka ‘kimanga’.
One Response to “ROSE MUHANDO APASUA NDOA YA MTU”
Sidhani kama rose muhando kila siku anadhambi yeye tu.nafahamu habari ya chuki binafsi, nadhani ndo inayoendelea hapa.Lakini namtia moyo rose asikate tamaa,pamoja na kuwa watu wanaona raha kuwanajisi wenzao na kuwapiga mawe mwisho wa siku mauti iko palepale.(Jipange sawa sawa)
Mungu akupiganie Rose.
Post a Comment