LULU, PACHA WA DOTNATA NDANI YA MBEYA AGOSTI 4,2013

WASANII WA FILAMU NCHINI ELIZABETH MICHAEL (LULU) NA PACHA WA DOTNA NI MIONGONI MWA WAGENI WATAKAOHUDHURIA TAMASHA LA KUITAMBULIA ALBAM YA NITANG’ARA TU YA MWINJILISTI KABULA GEORGE UTAKAOFANYIKA KATIKA MKOA WA MBEYA TAREHE 4 MWEZI WA 8, 2013. SEHEMU AMBAPO LITAFANYIKA TAMASHA HILO ITATANGAZWA HIVI KARIBUNI. WASILIANA NASI KWA SIMU NAMBA 0755 240136/0712001880.

JIPATIE SOFA SAFI KWA KOMBA SOFA SHOORM MKOANI MBEYA

KOMBA SOFA SHOORM (YESU NDIYE) NI WATENGENEZAJI WA SOFA ZA KISASA NA KUZIUZA KWA GHARA NAFUU SANA. WAPO MBEYA STRIRED JIRANI NA KANISA LA HIJA MWANJELWA JIRANI NA KANISA KUBWA WA ROMA. WASILIANA NAO KWA SIMU NAMBA 0754553467 AU 0655 553467. NYOTE MNAKARIBISHWA.

ECK PRODUCTION STUDIO YA KISASA NA KIMBILIO LA WAIMBAJI WA MUZIKI WA INJILI TANZANIA.



IPO MWEMBECHAI JIJINI DAR ES SALAAM, TANZANIA WAIMBAJI KAMA ROSE MUHANDO, HABATI BUKUKU, BONY MWAITEGE,UPENDO NKONE, JANGALA SON, MWANSASU NA WENGINE WENGI WAMEREKODIA KATIKA STUDIO HIYO. WASILIANA NAO KWA NAMBA +255 656 388 404

REDIO USHINDI FM KIPENZI CHA WATU WENGI NYANDA ZA JUU KUSINI

ROSE MUHANDO SAFARINI LOLIONDO


Malkia wa muziki wa Injili nchini, Rose Muhando, amedai kupanga safari ya kwenda  kijiji cha Samunge, wilayani Loliondo kukutana na Mchungaji, Ambilikile Mwasapile kwa lengo la kunywa dawa ili siku ya Tamasha la Pasaka linalotarajiwa kufanyika mwezi ujao limkute akiwa fiti.
Rose alitoa kauli hiyo hivi karibuni ndani ya  Studio za Zoom Production, zilizopo Magomeni Usalama jijini Dar es Salaam anakorekodia nyimbo zake kumi kwaajili ya albamu yake ya tatu.
Mkali wa Injili ambaye nyimbo zake huonekana mpya kila kukicha alisema kuwa, baada ya kupata taarifa ya tiba za Babu huyo alikuwa na mashaka nazo lakini kadiri siku zinavyokatika ameanza kuziamini kutokana na ushuhuda za watu mbalimbali wanaohudumiwa.
Endapo Rose atatekeleza adhima yake hiyo, atakuwa mwimbaji wa kwanza wa muziki huo kujitangaza kwenda kupata tiba kwa Babu wa Loliondo ambayo imekuwa ikiwagawa watumishi mbalimbali wa Mungu ambao kila mmoja amekuw akisema lake.


   

Newer Post Older Post