TAMASHA LA PASAKA KUVUNJA REKODI MWAKA HUU
Mkurugenzi wa Msama Promotions, Alex Msama amesema kuwa tamasha la Pasaka la mwaka huu linalotarajiwa kufanyika Sikukuu ya Pasaka Aprili 24 mwaka huu
kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee, Dar es Salaam, litavunja rekodi ya matamasha yote aliyowahi kuandaa.
kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee, Dar es Salaam, litavunja rekodi ya matamasha yote aliyowahi kuandaa.
Akizungumza na mtandao huu ndani ya ofisi zake jijini Dar es Salaam, Msama alisema kuwa kuvunja rekodi kwa tamasha hilo kunatokana na waimbaji waliodhibitisha kushiriki kuwa katika maandalizi mazuri na kila mmoja amekuwa na mda mzuri wa maombi kwa ajili ya kufanikisha shughuli hiyo.
Mgeni rasmi katika tamasha hilo anatarajiwa kuwa Rais, Jakaya Kikwete. Tamasha hilo litapambwa na waimbaji nguli wa nyimbo za kumsifu Mungu wakiongozwa na Rose Muhando.
Anawataja wasanii wengine wa nyimbo za Injili watakaopamba tamasha hilo ni Upendo Nkone, Bony Mwaitege, wanamuziki kutoka Kenya, Anastazia Mukabwa na Pamela Wanderwa na Mzambia, Ephraim Sekeleti aliothibitisha kushiriki.
Tamasha hilo lina malengo ya kuchangisha fedha kwa ajili ya watoto yatima, kuwasaidia
mitaji ya biashara wajane wasiojiweza na waathirika wa mabomu yaliyotokea kambi ya JWTZ Gongo la Mboto, Dar es Salaam, Februari 16 mwaka huu. Msama anasema kwa Dar es Salaam kiingilio kitakuwa Sh 4,000 kwa viti vya kawaida, viti vya maalumu (B) Sh 10,000 na viti maalumu (A) Sh 20,000. Tiketi za kategoria hiyo hazitauzwa mlangoni.
Tamasha la Pasaka la mwaka huu pia litashirikisha waimbaji wa nyimbo za Injili kutoka nchi sita ambazo ni Kenya, Uganda, Rwanda, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Afrika Kusini na Zambia. Pia kutakuwa na kwaya mbili kutoka katika nchi hizo.
Msama anasema msanii Sekeleti naye amekubali kushiriki na atatua nchini akiwa na albamu mpya iitwayo Mungu Mwenyewe. Anazitaja baadhi ya nyimbo zilizopo kwenye albamu hiyo kuwa ni Uniongoze na Kidonge cha Yesu.
Anasema Sekeleti atakuja nchini pamoja na waimbaji wake 10 na ataimba live siku hiyo.
Msama amesema kwamba tamasha la mwaka huu limekuwa na maboresha makubwa mno kwa ajili ya kukidhi matakwa ya wapendwa wengi.
“Kwanza kabisa tofauti na matamasha yaliyopita mwaka huu tutakuwa na waimbaji wengi zaidi wa muziki wa Injili kutoka nchi za nje,” anasema. “Waimbaji wote maarufu wa muziki wa Injili
watakuwepo, kwani tumejipanga vizuri mno kuhakikisha kwamba tamasha hili litakuwa gumzo kila mahali.
Post a Comment