LULU, PACHA WA DOTNATA NDANI YA MBEYA AGOSTI 4,2013

WASANII WA FILAMU NCHINI ELIZABETH MICHAEL (LULU) NA PACHA WA DOTNA NI MIONGONI MWA WAGENI WATAKAOHUDHURIA TAMASHA LA KUITAMBULIA ALBAM YA NITANG’ARA TU YA MWINJILISTI KABULA GEORGE UTAKAOFANYIKA KATIKA MKOA WA MBEYA TAREHE 4 MWEZI WA 8, 2013. SEHEMU AMBAPO LITAFANYIKA TAMASHA HILO ITATANGAZWA HIVI KARIBUNI. WASILIANA NASI KWA SIMU NAMBA 0755 240136/0712001880.

JIPATIE SOFA SAFI KWA KOMBA SOFA SHOORM MKOANI MBEYA

KOMBA SOFA SHOORM (YESU NDIYE) NI WATENGENEZAJI WA SOFA ZA KISASA NA KUZIUZA KWA GHARA NAFUU SANA. WAPO MBEYA STRIRED JIRANI NA KANISA LA HIJA MWANJELWA JIRANI NA KANISA KUBWA WA ROMA. WASILIANA NAO KWA SIMU NAMBA 0754553467 AU 0655 553467. NYOTE MNAKARIBISHWA.

ECK PRODUCTION STUDIO YA KISASA NA KIMBILIO LA WAIMBAJI WA MUZIKI WA INJILI TANZANIA.



IPO MWEMBECHAI JIJINI DAR ES SALAAM, TANZANIA WAIMBAJI KAMA ROSE MUHANDO, HABATI BUKUKU, BONY MWAITEGE,UPENDO NKONE, JANGALA SON, MWANSASU NA WENGINE WENGI WAMEREKODIA KATIKA STUDIO HIYO. WASILIANA NAO KWA NAMBA +255 656 388 404

REDIO USHINDI FM KIPENZI CHA WATU WENGI NYANDA ZA JUU KUSINI

MCHUNGAJI RWAKATARE ATOAMPYA BARAZA LA MAADILI

MBUNGE wa Viti maalum (CCM), Mchungaji Getrude Rwakatare jana alitoa mpya mbele ya Baraza la Maadili ya Viongozi wa Umma alikofikishwa kujieleza kwa nini hakujaza fomu ya kutangaza mali zake, baada ya kudai kuwa shetani ndiye amepoteza fomu hizo.Dk Rwakatare alisema hayo wakati akihojiwa na mwanasheria wa baraza hilo Getrude Cynacus.Katika utetezi wake, Dk Rwakatare alitumia maneno kama pepo, shetani na Mungu yalitawala.Mchungaji huyo alijitetea kuwa yeye alijaza fomu hizo na kuziwasilisha katika ofisi za bunge lakini hajui nini kilichotokea hadi fomu hizo zisifike kunakohusika.“Mambo mengine ni shetani tu, shetani ana nguvu sana kila mahali yuko,”alisema Mchungaji huyo na kuongeza kuwa:“Kazi yenyewe ya kujaza fomu ni ya dakika 10 tu sio kwamba unafanya mtihani Cambridge hivyo halikuwa zoezi kubwa kwangu hadi mimi nishindwe kujaza,”alisema.Alisema yeye hakuwa na wasiwasi kabisa kwamba angeweza kuwa mmoja wa watu ambao hawakujaza fomu hizo kwasababu alizijaza na kuzirejesha Ofisi ya Bunge.
Dk Rwakatare pia alionyesha nakala ya fomu hiyo anayodai kuijaza na kudai kuwa ana uzoefu wa muda mrefu katika fomu hizo na kwamba kila mwaka amekuwa akizijaza.“Tutaamini vipi kama nakala hiyo ni halali pengine ulikuwa nayo nyumbani na jana ukaitoa copy.

Je hukusaini kokote wakati uliporudisha fomu hizo?" alihoji mwanasheria wa baraza hilo Getrude Cynacus.Akijibu swali hilo Dk Rwakatare alisema wakati wa kuchukua fomu hizo ilikuwa lazima kusaini lakini kurudisha haikuwa lazima.

Baadhi ya mahojiano baina ya Mchungaji huyo na Mwanasheria huyo wa baraza yalikuwa hivi:Mwanasheria: Unasema ulijaza fomu, mbona hazikufika kwetu?Rwakatare: Hilo litakuwa ni pepo tu. Mimi nilirejesha na Mungu ni shahidi.Mwanasheria: Umeng’ang’ania shetani hivi huyo shetani ni nani?Rwakatare: Ni roho chafu ambaye kazi yake ni kuharibu na kufanya mambo yaende vibaya.Mwanasheria: Sasa huoni kama anakupeleka pabaya?Baada ya swali hilo, Mchungaji Rwakatare hakujibu kitu alikaa kimya.

Mwanasheria huyo aliliomba baraza hilo litupilie mbali utetezi wa Mchungaji huyo kwa sababu amekiri kutofanya ufuatiliaji.Hata hivyo akizungumza nje ya baraza hilo na waandishi wa habari, Dk Rwakatare alisema tangu uanze mchakato wa fomu hizo, hajasafiri kwenda mahali kokote na kwamba anashangaa kwanini hawakumpigia simu kumuuliza kama alijaza au la.“Mimi sijasafiri kwenda kokote na wala nilikuwa sina wasiwasi kabisa kwa sababu nilijaza fomu na kuzirejesha, wangeweza kunipigia simu na ningeweza kuja,”alisema.

Alipoulizwa na waandishi wa habari haoni kama kuna haja ya kuwakemea mashetani, Mchungaji huyo hakujibu kitu aliamua kuingia kwenye gari yake na kuondoka.Katika hatua nyingine, Mbunge wa Mpanda Vijijini kupitia CCM, Moshi Kakoso naye alifikishwa kwenye baraza hilo jana na kuitupia lawama ofisi ya bunge kwa madai kuwa alijaza fomu na kuzikabidhi kwa wahudumu wa ofisi hiyo.“Sijafurahia kuitwa katika baraza hili ni kitendo ambacho si kizuri.

Naomba nipewe nafasi ya kujaza fomu nyingine ili nitekeleze sheria za nchi,”alisema Kakoso.Alisema yeye hana mali za kutisha kiasi cha kumfanya ashindwe kujaza fomu hizo na kulalamikia ofisi ya bunge kuwa haiko makini katika utunzaji wa kumbukumbu.

Mbunge huyo pia alipoulizwa na Mwenyekiti wa baraza hilo Jaji Damian Lubuva kuhusu kumpa muhudumu wa ofisi ya bunge nyaraka muhimu kama hizo, alijitetea kuwa hilo ni bunge lake la kwanza na kwamba alidhani kuwa alikuwa sahihi kumpa muhudumu huyo.

“Hata mawasiliano ya barua kuja Mpanda yanachukua muda mrefu sana na kutufanya sisi wengine tuonekane tumekiuka sheria,”alisema Kakoso.Baada ya kusikiliza utetezi wa wabunge hao, Jaji Lubuva alisema watatoa uamuzi na mapendekezo yao kwenye mamlaka zinazohusika.Baraza hilo litaendelea leo ambapo Mbunge wa Mbinga Magharibi John Komba, diwani kutoka Geita Elias Okomu na Hakimu wa Mahakama ya Mwanzo Sumbawanga Edwin



HABARI HII NI KWA MUJIBU WA GAZETI LA MWANANCHI

Newer Post Older Post