LULU, PACHA WA DOTNATA NDANI YA MBEYA AGOSTI 4,2013

WASANII WA FILAMU NCHINI ELIZABETH MICHAEL (LULU) NA PACHA WA DOTNA NI MIONGONI MWA WAGENI WATAKAOHUDHURIA TAMASHA LA KUITAMBULIA ALBAM YA NITANG’ARA TU YA MWINJILISTI KABULA GEORGE UTAKAOFANYIKA KATIKA MKOA WA MBEYA TAREHE 4 MWEZI WA 8, 2013. SEHEMU AMBAPO LITAFANYIKA TAMASHA HILO ITATANGAZWA HIVI KARIBUNI. WASILIANA NASI KWA SIMU NAMBA 0755 240136/0712001880.

JIPATIE SOFA SAFI KWA KOMBA SOFA SHOORM MKOANI MBEYA

KOMBA SOFA SHOORM (YESU NDIYE) NI WATENGENEZAJI WA SOFA ZA KISASA NA KUZIUZA KWA GHARA NAFUU SANA. WAPO MBEYA STRIRED JIRANI NA KANISA LA HIJA MWANJELWA JIRANI NA KANISA KUBWA WA ROMA. WASILIANA NAO KWA SIMU NAMBA 0754553467 AU 0655 553467. NYOTE MNAKARIBISHWA.

ECK PRODUCTION STUDIO YA KISASA NA KIMBILIO LA WAIMBAJI WA MUZIKI WA INJILI TANZANIA.



IPO MWEMBECHAI JIJINI DAR ES SALAAM, TANZANIA WAIMBAJI KAMA ROSE MUHANDO, HABATI BUKUKU, BONY MWAITEGE,UPENDO NKONE, JANGALA SON, MWANSASU NA WENGINE WENGI WAMEREKODIA KATIKA STUDIO HIYO. WASILIANA NAO KWA NAMBA +255 656 388 404

REDIO USHINDI FM KIPENZI CHA WATU WENGI NYANDA ZA JUU KUSINI

MWINJILISTI KABULA; NYOTA INAYONG’ARA KATIKA MUZIKI WA INJILI

MWINJILISTI KABULA AKIIMBA PAMOJA NA MWANAYE KUSHOTO GLORY GEORGE
Kila ukisikiliza matangazo ya mikutano na matamasha ya dini utasikia majina ya waimbaji wa muziki wa injili kama Bony Mwaitege, Bahati Bukuku, Upendo Nkone na Martha Mwaipaja kuwa watahudumu kwa njia ya uimbaji.
Waimbaji hao wamejikusanyi mashabiki wengi kutokana na uzuri wa nyimbo zao na kibali walichonacho mbele ya mashabiki wao.
Jina la Mwinjilisti Kabula George naamini si geni masikioni mwa wapenzi wa muziki wa injili kwani ameanza kuimba kitambo kidogo. Mwinjilisti Kabula alianza rasmi kujishughulisha na kazi ya muziki wa injili mwaka 2005 baada ya kutoa albamu yake ya kwanza iliyoitwa ‘Pesa’.
Baada ya hapo alitoka na albamu ya ‘Ushindi’ na sasa anang’ara na albamu yake ya tatu iitwayo ‘Nitang’ara tu’ iliyokatika mfumo wa DVD.
Hivi karibuni nilipata nafasi ya kufanya naye mahojiano na alinieleza mambo mengi na alieleza kwa undani kuhusu historia yake kimuziki.
Nini kilimvutia katika fani ya muziki huo?
“Ikumbukwe kuwa injili ni uweza wa Mungu uletao wokovu kwa kila aaminiye. Huduma hii niliipenda tangu utotoni kipindi hicho nilikuwa naabudu katika kanisa Katoliki nyumbani kwetu Kwimba. Nilishawishika kuwa mwimbaji wa muziki huo baada ya kuvutiwa na uimbaji wa kwaya ya kanisani hapo”.
Je ni kweli waimba injili wameugeuza muziki huo kuwa biashara?
Watu wengi wamekuwa wakizungumzia suala hilo, hivyo mimi siwezi kukanusha wala kukubaliana na hoja yao hiyo. Inawezekana ni kweli wanavyosema na hii inatokea kila mwimbaji kuwa na mtazamo wake kihuduma.
Leo hii watu wamegawanyia. Hata midundo ya baadhi ya nyimbo wanasema ni ya ‘kidunia’ hasa ukiwa unaimba huku unacheza kwa kujituma. Ieleweke kuwa baadhi ya watu hata kupiga makofi tu wakati unaimba kwao ni “kidunia”.
Binafsi sioni ubaya wowote wa kumuimba Mungu kwa midundo hiyo kwani hata wadau wa muziki wa injili nao wamegawanyika. Wapo wanaopenda nyimbo zenye midundo na wengine hawapendi, hivyo ili kuwahubiria wote ni vema tukawa na midundo ya aina yote.
Je, ni kweli sauti yake ameiga kwa Bahati Bukuku?
Watu wengi wanasema nimemuiga Bahati Bukuku, kimsingi tunatofautiana na kila mmoja ana uimbaji wake kwa kadiri ya kipawa au kipaji alichopewa na Mungu. Wanaosema kuwa namwiga mwimbaji huyo wanakosea. Ni muige ili iweje. Nampenda sana Bahati na penda pia uimbaji wake sema tu imetokea sauti zetu kufanana.
Changamoto zipi anakabiliana nazo katika utumishi wake?
Changamoto ni nyingi miongoni mwa hizo ni suala la wizi wa kazi zangu jambo ambalo linanirudisha nyuma kimaendeleo kwa kunikosesha mapato.
Ni wimbo gani anaupenda kuliko zote?
Namshukuru Mungu nazipenda nyimbo zangu zote kwani huwa nazituka kutokana na uvuvio wa ngungu ya Roho Mtakatifu hivyo itakuwa ni jambo la ajabu kuzibagua hapo itakuwa sawa na kumkufuru Roho Mtakatifu.
Kuna tofauti ngani za kimsingi kati ya muziki wa injili na wa Bongo Fleva?
Kuna tofauti kuwa sana ujumbe wa muziki wa Injili unaelekeza kujenga roho ya mtu ama kumpa matumaini ya kuishi kama alikuwa amekata tama wakati Bongo fleva asilimia kubwa unalenga katika mambo yahusuyo mwili zaidi na mara nyingi unapotosha roho ya mtu.
Asilimia kubwa ya nyimbo hizo zinahamasisha ngono, kuutukuza mwili, kujisifia, kusifia wanawake nk.
Nini mipango yake kwa mwaka huu?
Nina mpango wa kulihubiri zaidi neno la Mungu ndani na nje ya nchi na nitafanya hivyo kadiri Mungu atakavyoniongoza.
Video yake ya Nitang’ara tu imepokelewaje na mashabiki wake?
Namshukuru Mungu kuwa imepokelewa vizuri na sasa inapatikana katika maduka yote ya kanda nchini. Napokea simu nyingi zana za mialiko ya kwenda kuhudumu mikoa mbalimbali na hiyo ni baada ya kuona uweza wa nguvu ya Mungu uliomo ndani ya nyimbo hizo.
DVD yangu ina nyimbo sita ambazo kila wimbo unaradha yake. Nyimbo hizo ni Nitang’ara tu, Majaribu, Nimesogea, Nataka kumuona Yesu, Ni mwema na Peleleza.

Newer Post Older Post