MIRIAM LUKINDO MAUKI KUITEKA MATEMBELE YA PILI
MIRIAM NA MUMEWE |
Mwimbaji wa muziki wa injili nchini, Miriam Lukindo Mauki ‘Binti Afrika’ Jumamosi hii atatarajiwa kuitaka Matembele ya Pili atakapokuwa anashiriki uzinduzi wa albamu mbili za kwaya ya Sauti za Sifa iliyo chini ya Huduma ya The Word of Reconciliation Ministries (WRM).
Akizungumza na TGM leo jijini Dar es Salaam, mwalimu wa kwaya hiyo, Elibariki Isango alisema Miriam amekubali kuungana nao na siku hiyo atapanda jukwaa moja na Christina Shusho kuimba wakati wa uzinduzi albamu zao hizo ambazo ni Enendeni kwa Roho na Pokea Sifa.
“Miriam amekubali kuja kutuunga mkono katika shughuli yetu ya kuzindua albamu zetu mbili na ataungana na Shusho kuimba nyimbo zao mbalimbali hivyo naomba wakazi wote wa Dar es Salaam na vitongoji vyake kufika kwa wingi kwenye uzinduzi huo,” alisema Isango.
Mwalimu Isango alisema kuwa lengo la uzinduzi wa albamu hizo ni kukusanya fedha kwa ajili ya kumalizia ujenzi wa jengo la huduma hiyo ambalo kwa sasa lipo katika hatua za mwisho hivyo kila atakayefika katika uzinduzi huo na kununua CD zao atakuwa ametoa sadaka yake ya kukamilisha hekalu la Bwana.
Waimbaji wengine watakaoimba kwenye uzinduzi huo ni Ami Mwakitalu, Madamu Luti & Chris, Faraja Moleli, Queen Talaba, Wilson John, Magreth na wengine wengi na shughuli itaanza majira ya saa 6:00 mchana na kumalizika saa 12 jioni.
Mwalimu Isango alimaliza kwa kusema kuwa hakutakuwa na kiingilio katika uzinduzi huo hivyo wadau wa muziki wa injili hasa wanaoishi maeno ya Kitunda, Ukonga na Gongolamboto kufika kwa wingi kwani hiyo ni mara ya kwanza kwa waimbaji kama Shusho na Miriam kuimba eneo hilo.
Post a Comment