LULU, PACHA WA DOTNATA NDANI YA MBEYA AGOSTI 4,2013

WASANII WA FILAMU NCHINI ELIZABETH MICHAEL (LULU) NA PACHA WA DOTNA NI MIONGONI MWA WAGENI WATAKAOHUDHURIA TAMASHA LA KUITAMBULIA ALBAM YA NITANG’ARA TU YA MWINJILISTI KABULA GEORGE UTAKAOFANYIKA KATIKA MKOA WA MBEYA TAREHE 4 MWEZI WA 8, 2013. SEHEMU AMBAPO LITAFANYIKA TAMASHA HILO ITATANGAZWA HIVI KARIBUNI. WASILIANA NASI KWA SIMU NAMBA 0755 240136/0712001880.

JIPATIE SOFA SAFI KWA KOMBA SOFA SHOORM MKOANI MBEYA

KOMBA SOFA SHOORM (YESU NDIYE) NI WATENGENEZAJI WA SOFA ZA KISASA NA KUZIUZA KWA GHARA NAFUU SANA. WAPO MBEYA STRIRED JIRANI NA KANISA LA HIJA MWANJELWA JIRANI NA KANISA KUBWA WA ROMA. WASILIANA NAO KWA SIMU NAMBA 0754553467 AU 0655 553467. NYOTE MNAKARIBISHWA.

ECK PRODUCTION STUDIO YA KISASA NA KIMBILIO LA WAIMBAJI WA MUZIKI WA INJILI TANZANIA.



IPO MWEMBECHAI JIJINI DAR ES SALAAM, TANZANIA WAIMBAJI KAMA ROSE MUHANDO, HABATI BUKUKU, BONY MWAITEGE,UPENDO NKONE, JANGALA SON, MWANSASU NA WENGINE WENGI WAMEREKODIA KATIKA STUDIO HIYO. WASILIANA NAO KWA NAMBA +255 656 388 404

REDIO USHINDI FM KIPENZI CHA WATU WENGI NYANDA ZA JUU KUSINI

SHUSHO KUNOGESHA UZINDUZI WA SAUTI ZA SIFA


Mwimbaji wa muziki wa Injili nchini, Christina Shusho anatarajiwa kunogesha uzinduzi wa albamu mbili kwa mpigo za kwaya ya nyimbo za kusifu na kuabudu iitwayo Sauti za Sifa ya Huduma ya The Word of Reconciliation Ministries (WRM) iliyopo Matembele ya Pili Kivule jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na TGM leo jijini Dar es Salaam, mwalimu wa kwaya hiyo Elibariki Isango alisema kuwa Shusho amethibitisha kushiriki katika uzinduzi huo ambao alidai utakuwa wa kihistoria katika eneo hilo.
“Shusho amekubali kuja kutuunga mkono katika uzinduzi huo unaotarajiwa kufanyika Agosti 25 mwaka huu ndani ya Ukumbi wa WRM kuanzia majira ya saa nne asubihi,” alisema Isango.
Isango alizitaja albamu hizo kuwa ni Heshima na Utukufu na Enendeni kwa Roho zikiwa katika mfumo wa CD na hakutakuwa na kiingilio siku hiyo.
Aliongeza kuwa mbali na Shusho waimbaji wegine wa muziki huo kutoka na Dar es Salaam na Arusha wataimba na sasa anafanya mazungumzo nao na mambo yakiwa tayari atawajulisha wadau wa muziki huo.
Isango alimaliza kwa kusema kuwa fedha zitakazopatikana katika uzinduzi huo zitatumika kumalizia ujenzi wa jengo la huduma hiyo ambalo lipo katika hatua za mwisho za kukamilika.

Newer Post Older Post