LULU, PACHA WA DOTNATA NDANI YA MBEYA AGOSTI 4,2013

WASANII WA FILAMU NCHINI ELIZABETH MICHAEL (LULU) NA PACHA WA DOTNA NI MIONGONI MWA WAGENI WATAKAOHUDHURIA TAMASHA LA KUITAMBULIA ALBAM YA NITANG’ARA TU YA MWINJILISTI KABULA GEORGE UTAKAOFANYIKA KATIKA MKOA WA MBEYA TAREHE 4 MWEZI WA 8, 2013. SEHEMU AMBAPO LITAFANYIKA TAMASHA HILO ITATANGAZWA HIVI KARIBUNI. WASILIANA NASI KWA SIMU NAMBA 0755 240136/0712001880.

JIPATIE SOFA SAFI KWA KOMBA SOFA SHOORM MKOANI MBEYA

KOMBA SOFA SHOORM (YESU NDIYE) NI WATENGENEZAJI WA SOFA ZA KISASA NA KUZIUZA KWA GHARA NAFUU SANA. WAPO MBEYA STRIRED JIRANI NA KANISA LA HIJA MWANJELWA JIRANI NA KANISA KUBWA WA ROMA. WASILIANA NAO KWA SIMU NAMBA 0754553467 AU 0655 553467. NYOTE MNAKARIBISHWA.

ECK PRODUCTION STUDIO YA KISASA NA KIMBILIO LA WAIMBAJI WA MUZIKI WA INJILI TANZANIA.



IPO MWEMBECHAI JIJINI DAR ES SALAAM, TANZANIA WAIMBAJI KAMA ROSE MUHANDO, HABATI BUKUKU, BONY MWAITEGE,UPENDO NKONE, JANGALA SON, MWANSASU NA WENGINE WENGI WAMEREKODIA KATIKA STUDIO HIYO. WASILIANA NAO KWA NAMBA +255 656 388 404

REDIO USHINDI FM KIPENZI CHA WATU WENGI NYANDA ZA JUU KUSINI

COSOTA HUU NI WAKATI WA KUONESHA MAKUCHA YENU

Jana serikali kupitia Naibu Waziri wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Amos Makalla iliyahakikishia Mashirikisho ya Sanaa nchini kuwa kuanzia Januari Mosi 2013 itaanza kuziwekea stika kazi zote kwa lengo la kuondoa uharamia uliokuwa unafanywa na watu wachache waliokuwa wajitajirisha kupitia migongo ya wasanii.

Kwa muda mrefu sasa kumekuwa hakuna sheria kali ya kuwabana maharamia wanaojinufaisha na kazi hizo huku Chama Cha Haki Miliki Tanzania (COSOTA) kikishindwa kusaidia chochote juu suala hilo.

Baadhi ya maharamia  waliokamatwa hakuna hata mmoja aliyefungwa kwa kosa hilo na tatizo la kuibiwa kazi hizo linaongezeka kila kukicha.

Mara nyingi COSOTA walikuwa wanasema hakuna sheria kali ambayo inaweza kuwafanya maharamia hao wasifanye upuuzi waliokuwa wanaufanya kwa miaka mingi na kuwaacha wasanii wakitabika huku kazi zao zikiuzwa kama njugu mitaani.

 Wizara tatu zimeungana kuhakikisha suala hili linakomeshwa ambapo zitarasimisha kazi hizo kwa kuziwekea stika. Wizara hizo ni Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Wizara ya Viwanda na Biashara pamoja na Wizara ya Fedha lengo ni kuhakikisha tatizo hilo linakomeshwa.

Muungano huo uwape mwanja COSOTA kuonesha makucha yenu kwani mnatuhumiwa kulipwa mishahara minono na baadhi ya maharamia ndiyo maana mumeshindwa kudhibiti tatizo hili kwa muda mrefu sasa.

Pia hii isiwe siasa kwa suala hili kwani mara nyingi Watanzania ni wazuri kwa maneno lakini utekelezaji hakuna. Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) ambayo ndiyo itakuwa inatoa stika nayo isiingie kwenye skendo ya COSOTA kwa kutoa stika kinyemela kwa maharamia hao kwa  kuwazunguka wasanii.

Endapo TRA itasimamia vizuri zoezi hili, itajipatia fedha nyingi ambazo zimekuwa zikipotea kwani wasanii watawajibika kulipa kodi ya mapato.

Itakuwa ni ajabu msanii analipa kodi ya mapato lakini kazi yake inaibiwa na TRA waonekane kukosa meno kama COSOTA. Kwani kwa muda wote huo mimi sijaona umuhimu wa uwepo wa COSOTA hapa nchini.

Lakini hii pia ni nafasi nzuri kwa wizara hizi kama kweli zitafanikisha kukomesha tatizo hili viongozi walio madarakani sasa wataingia kwenye historia ya kukomesha ujangili huu ambao umekuwa suku miaka mingi.

Newer Post Older Post