SARAH AWASHANGAA WAIMBA INJILI
Mwimbaji wa nyimbo za injili nchini,
Sarah Sanga amewashangaa waimbaji wenzake kwa kushindwa kujitokeza kwa wingi
kusajili kazi zao katika Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA) na Chama Cha Haki
Milikimiliki Tanzania (COSOTA) kisha kwenda kuwekewa stika na Mamlaka ya Mapato
Tanzania (TRA) kwa ajili ya ulinzi wa kazi zao siibiwe.
Akizungumza na gazeti hili jana jijini
Dar es Salaam, Sarah alisema kuwa huu ni wakati mzuri kwa waimbaji wa muziki wa
injili kujitokeza kwa ajili ya kusajili na wasisubiri mpaka zoezi liwe kugumu
kutokana na foleni ambayo inaweza kujitokeza kwa siku zijazo.
“Unajua Watanzania tumezoea mpaka
kusubiri mpaka siku ya mwisho ndipo tujazane kwenye kujisajili, naomba kabla
mambo hayajawa mazito twende kusajili kazi zetu, japo najua zoezi hili halina
kikomo lakini ni vema kwenda mapema,” alisema Sarah.
Sarah anayetamba na wimbo wake wa
Simama Unitetee Baba amesema kuwa binafsi yeye wiki hii anaenda kusajili kazi
yake sehemu husika ili awe na uhuru wa kuisambaza kazi yake kwa uhakika wa
kutoibiwa na wajanja wachache ambao kwa asimilia kubwa wamejinemesha kupitia
migongo ya wasanii bila kuvuja jasho.
Tayari
serikali imesema kuanzia mwezi huu kazi zote za sanaa zinatakiwa kuwa na stika
kutoka TRA na imeweka utaratibu wa wasambazaji wote wa kazi za wasanii
kubandika stika ya usalama ijulikanayo kama Hakigram kwenye kila nakala ya kazi
itakayosambazwa, ili kuhakikisha kazi za wasanii haziibwi.
Serikali imeagiza kuwa kila msambazaji ataingia mkataba na msanii
kusambaza idadi fulani ya nakala na kupewa stika za Hakigram ambazo zitabandikwa kila nakala na kazi ambazo hazina stika zitatambuliwa kama nakala bandia na kuondolewa katika soko.
Serikali imeagiza kuwa kila msambazaji ataingia mkataba na msanii
kusambaza idadi fulani ya nakala na kupewa stika za Hakigram ambazo zitabandikwa kila nakala na kazi ambazo hazina stika zitatambuliwa kama nakala bandia na kuondolewa katika soko.
Post a Comment