Kila kukicha ukifungua vituo vya radio za dini hapa nchini, utasikia matangazo ya matamasha yakitangazwa kwa lengo la uzinduzi wa albamu za waimbaji wa muziki wa injili.
Ukichunguza kwa undani zaidi juu ya matamasha hayo, utabaini kwamba, waandaaji hulenga kujipatia fedha za chapuchapu ili wajinasue na dimbwi la umasikini.
Nasema hivyo nikiwa na ushahidi kwamba baadhi ya waimbaji wa muziki wa injili miaka hii wamekuwa wakitunga nyimbo zao kwa kuangalia ni kwa jinsi gani watachomoza katika anga la muziki huo.
Safu hii, ilifanikiwa kuzungumza na mwimbaji wa muziki huo Papa Jonas Lutumba, ambaye naye bila kuficha alisema kuwa watu hao miaka ya hivi karibuni, wameibuka kama uyoga na kuwafanya waimbaji wa muziki huo waangushiwe shutuma yakuwa wamekuwa wakipenda fedha zaidi kuliko kuangalia huduma.
Papa alisema kuwa, kitendo cha waimbaji hao wanaoibukia katika fani hiyo kuanza tabia ya kutanguliza fedha badala ya kuangalia huduma ya Mungu, kunaidhalilisha uimbaji na kuonekana haina heshima katika jamii.
Mwimbaji huyo ambaye ni raia wa Jamhuri ya Demokrasia ya Kongo (DRC Congo), anayeishi hapa nchini alisema kuwa, waimbaji hao, wamekuwa waiipaka matopete huduma ya muziki wa injili na kuonekana si kitu, na ndio maana mifano mingi mibaya, watu wengi wamekuwa wakiwatolea watumishi hao wa Mungu.
Akizungumzia historia yake ya wokovu, Papa alisema, huduma ya kumuimbia Mungu wake alianza mwaka 1996 baada ya kuokoka. Hata hivyo si kwamba uimbaji ulianza mwaka huo, la hasaha, bali kabla ya wokovu alikuwa akiimba katika bendi ya Mosha Star ya DRC Congo mwaka 1990.
Papa Lutumba tayari amefanikiwa kurekodi albamu tatu ambazo tayari ziko sokoni. Albamu hizo ni Mungu wangu aliyoitoa mwaka 2004, Wakati wa Neema aliyoirekodi mwaka 2006 na Nikumbuke aliyoifyatua mwishoni mwa mwaka jana.
Akizungumza na safu ya Gospel Fleva Papa alisema albamu yake ya tatu inayokwenda kwa jina la Unikumbuke, mwanzoni mwa mwezi Fabruari inatarajiwa kuingia mtaani ikiwa katika DVD, VCD na VHS na maandalizi yote yamekamilika.
Akielezea juu kuhusu mauzo ya kazi za muziki wa injili, Papa alisema kwa Tanzania soko si kubwa sana ukilinganisha na nchi kama Kenya na Kongo, kutokana na ukosefu wa ushindani wa wasambazaji wa kazi hizo.
Hata hivyo Papa alisema kwamba Waimbaji wa muziki wa Tanzania wao wanafaida kubwa ya kuwa na studio nyingi za kurekodia muziki tofauti na Kongo ambapo studio ni chache hali ambayo husababisha kazi ya kurekodi kuwa ngumu.
One Response to “PAPA JONAS LUTUMBA KUIPUA DVD,VCD & VHS”
Huyu ni mbwa mwitu ambaye anajifunika katika manyoya ya kondoo. Sasa hivi yupo katika mpango wa kurubuni wazee waumini wauze nyumba yake na yeye achukue hapo shs milioni mia moja. Nasema ASHINDWE katika mbinu zake hizo za kishetani. Roho Mtakatfu wa Mungu ataangaza nuru yake dhidi ya hawa manabii wa uongo wanaokuja kuhubiri kutoka mbali kwa jina lake.
Post a Comment