ALBAMU YA USHINDI KUINGIA SOKONI MWEZI UJAO
Albamu ya Ushindi ya muimbaji wa muziki wa Injili nchini Kabula George, inatarajiwa kuingia sokoni mwezi ujao baada ya wapenzi wa muziki huo kuwa na kiu kubwa ya kuisikiliza kwa ukaribu zaidi kuliko ilivyo sasa ambapo nyimbo zake wanazisikiliza radioni na kukutana naye katika ziara zake anazozifanya jijini Dar es Salaa kwa lengo la kuitambulisha.
Akizungumza na kona hii jana jijini Dar, Kabula alisema kuwa awa ilikuwa aiingize sokoni albamu hiyo mwishoni mwa mwezi ujao, lakini kutokana na watu wengi kuzihitaji nyimbo zake amelazima kuzitoa mapema ili wapate vema ujumbe uliomo ndani yake.
“Nimelazimika kuiingiza sokoni albamu yangu ya Ushindi kutokana na wapenzi wa muziki wa Injili kuwa na kiu kubwa ya kuzisikiliza nyimbo zangu kwa ukaribu zaidi kuliko ilivyo sasa ambapo wanazikiliza kupita vituo vya radio,” alisema Kabula.
Mwimbaji huyo ambaye ameonekana kuteka mioyo ya wapenzi wa muziki nchini, alisema haoni haja ya kuendelea kusubiri mpaka mwisho wa mwezi ujao huku watu wakionyesha dhahili kuzikubali nyimbo zake.
Akizungumza na safu hii hivi karibuni, Kabula alisema kuwa, licha ya kuwa ni siku ya sikukuu ya Pasaka, analazimika kufanya hivyo ikiwa ni moja ya ziara yake ya kuitambulisha albamu yake katika jiji la Dar es Salaam kabla ya kwenda mikoani.
Kabula aliwataka wakazi wote wa Temeke na maeneo jirani wenye shida na matatizo mengi yanayowakumba wafike kwa wingi katika ukumbi huo ili wakutane na nguvu za Mungu ambazo zimekuwa zikiwashukia watu wengine ambao wamefanikiwa kuabudu pamoja naye katika makanisa tofauti kwa siku za hivi karibuni.
Alisema kuwa, siku hiyo Mungu atadhihirisha uweza na nguvu zake kwa watu wote wanaosumbuliwa na nguvu za giza ikiwa ni pamoja na kwa akina mama wasiobahatika kupata watoto na kubezwa na ndugu jamaa na marafiki.
“Nyimbo zangu zimekuwa na utofauti mkubwa na waimbaji wengine kwa sababu wagonjwa wengi wamekuwa wakipona magonjwa yao ikiwa ni pamoja na kufunguliwa nguvu za giza ambazo zinawasumbua kwa muda mrefu pindi ninapokuwa naimba, na kama hawaamini waje PTA washuhudie hiki ninachokisema,” alisema Kabula.
Post a Comment