LULU, PACHA WA DOTNATA NDANI YA MBEYA AGOSTI 4,2013

WASANII WA FILAMU NCHINI ELIZABETH MICHAEL (LULU) NA PACHA WA DOTNA NI MIONGONI MWA WAGENI WATAKAOHUDHURIA TAMASHA LA KUITAMBULIA ALBAM YA NITANG’ARA TU YA MWINJILISTI KABULA GEORGE UTAKAOFANYIKA KATIKA MKOA WA MBEYA TAREHE 4 MWEZI WA 8, 2013. SEHEMU AMBAPO LITAFANYIKA TAMASHA HILO ITATANGAZWA HIVI KARIBUNI. WASILIANA NASI KWA SIMU NAMBA 0755 240136/0712001880.

JIPATIE SOFA SAFI KWA KOMBA SOFA SHOORM MKOANI MBEYA

KOMBA SOFA SHOORM (YESU NDIYE) NI WATENGENEZAJI WA SOFA ZA KISASA NA KUZIUZA KWA GHARA NAFUU SANA. WAPO MBEYA STRIRED JIRANI NA KANISA LA HIJA MWANJELWA JIRANI NA KANISA KUBWA WA ROMA. WASILIANA NAO KWA SIMU NAMBA 0754553467 AU 0655 553467. NYOTE MNAKARIBISHWA.

ECK PRODUCTION STUDIO YA KISASA NA KIMBILIO LA WAIMBAJI WA MUZIKI WA INJILI TANZANIA.



IPO MWEMBECHAI JIJINI DAR ES SALAAM, TANZANIA WAIMBAJI KAMA ROSE MUHANDO, HABATI BUKUKU, BONY MWAITEGE,UPENDO NKONE, JANGALA SON, MWANSASU NA WENGINE WENGI WAMEREKODIA KATIKA STUDIO HIYO. WASILIANA NAO KWA NAMBA +255 656 388 404

REDIO USHINDI FM KIPENZI CHA WATU WENGI NYANDA ZA JUU KUSINI

BARAKA FRANCIS MWIMBAJI WA MUZIKI WA INJILI ALIYEJIKITA KWENYE UPRODYUZA






UIMBAJI wa muziki wa Injili nchini umeonekana kushika kasi ya ajabu kutokana na wazee kwa vijana kujitumbukiza katika huduma hiyo takatifu ya kulihubiri Neno la Mungu kwa njia hiyo.
Watu wengi wameguswa na huduma hiyo mara baada ya kuona baadhi yao licha ya kutokuwa na elimu ya kutosha lakini muziki umewatoa kimaisha na kuwa sawa na waliosoma.Hali hiyo ndiyo imepelekea kila kukicha  watu wakiwa wanapanga foleni kwenda studio kuangalia gharama ya kurekodi na wengine wakiwa katika mazoezi makali ya kujiandaa kwenda studio.Ukidhani nakudanganya, funga safari sasa hivi uende kwenye studio za kurekodi kama hutakuta vijana kwa wazee wakipishana mlangoni kuangalia kama kazi zao zimekamilika na wengine ndiyo wanaweka 
‘booking’ ya kupangiwa siku ya kwenda kufanya hivyo.
Lakini pamoja na mwamko huo wa watu kupenda huduma ya utumishi kwa njia ya uimbaji, wengi wao hawajui kutumia vyombo vya muziki ambavyo vinaweza kuwawezesha kupata muziki mzuri wanaoupata, na hujikuta wanaishia kupigiwa ala ambazo hawazipendi ama ziko nje ya matakwa yao. Baadhi ya waimbaji huwa wanaenda studio wakiwa na ala zao kichwani ambazo huwaongoza katika kuimba vyema wimbo walioutunga. Lakini ndoto za muziki wao mara nyingi hujikuta zinapotea pindi wanapofika kwa mtaalamu wa kutengeneza muziki ambaye naye hupiga kama anavyojisikia yeye mwenyewe. Tatizo hilo aliliona mapema muimbaji wa muziki wa Injili nchini, Baraka France, aliyevuma miaka ya nyuma na kibao chake cha Unishike alichokiimba kwa hisia kali na kusababisha kila mtu kupenda kukisikiliza mchana na usiku. Kibao hicho hata leo kikipigwa watu wengi huwa wanabarikiwa nacho. Baraka si jina geni kwa wapenzi wa radio za dini nchini ambao wamekuwa wakipata mguso wa ajabu kupitia nyimbo hizo. Alianza muziki akiwa kinda, na mwaka 1997 alianza rasmi huduma ya uimbaji akiwa katika kanisa la Tanzania Assemblies of God (TAG) Ubungo jijini Dar es Salaam, na mwaka 1999 alijiunga na bendi ya Union for the Gospel Ministries. Akiwa katika bendi hiyo alianza kujifunza kupiga vyombo vya muziki na kufanikiwa kwa kiwango cha juu. Baada ya kuimudu vema kazi ya kupiga vyombo vya muziki, alijifunza uprodyuza na mwaka 2004 alijiunga na studio ya Malaika iliyopo Kinondoni jijini Dar es Salaam na kufanikiwa kutunga wimbo wa Jina la Yesu aliowapa vijana wa kundi la Furaha (Furaha Group) kabla ya kuijunga na studio ya JAG Records na kisha kufyatua kibao chake binafsi alichokipa jina la Unishike hiyo ikiwa ni mwaka 2008. Tayari mtumishi huyo wa Mungu amerekodi albamu yake ya pili inayokwenda kwa jina la Ulisema Nikukumbushe yenye vibao vinane aliyoirekodia katika studio ya Zion iliyopo Kimara Bucha jijini Dar es Salaam huku video yake ikirekodiwa katika studio ya Yakwetu Media. Mwanamuziki huyo ambaye amejikita zaidi katika kazi ya uprodyuza, alimaliza kwa kuvishukuru vyombo vya habari hasa vya dini kwa kukuza muziki wa Injili nchini pamoja na Kampuni ya Global Publishers ambayo imekuwa mbele kufanya kazi pamoja na wasanii mbalimbali wa muziki huo.

Newer Post Older Post