LULU, PACHA WA DOTNATA NDANI YA MBEYA AGOSTI 4,2013

WASANII WA FILAMU NCHINI ELIZABETH MICHAEL (LULU) NA PACHA WA DOTNA NI MIONGONI MWA WAGENI WATAKAOHUDHURIA TAMASHA LA KUITAMBULIA ALBAM YA NITANG’ARA TU YA MWINJILISTI KABULA GEORGE UTAKAOFANYIKA KATIKA MKOA WA MBEYA TAREHE 4 MWEZI WA 8, 2013. SEHEMU AMBAPO LITAFANYIKA TAMASHA HILO ITATANGAZWA HIVI KARIBUNI. WASILIANA NASI KWA SIMU NAMBA 0755 240136/0712001880.

JIPATIE SOFA SAFI KWA KOMBA SOFA SHOORM MKOANI MBEYA

KOMBA SOFA SHOORM (YESU NDIYE) NI WATENGENEZAJI WA SOFA ZA KISASA NA KUZIUZA KWA GHARA NAFUU SANA. WAPO MBEYA STRIRED JIRANI NA KANISA LA HIJA MWANJELWA JIRANI NA KANISA KUBWA WA ROMA. WASILIANA NAO KWA SIMU NAMBA 0754553467 AU 0655 553467. NYOTE MNAKARIBISHWA.

ECK PRODUCTION STUDIO YA KISASA NA KIMBILIO LA WAIMBAJI WA MUZIKI WA INJILI TANZANIA.



IPO MWEMBECHAI JIJINI DAR ES SALAAM, TANZANIA WAIMBAJI KAMA ROSE MUHANDO, HABATI BUKUKU, BONY MWAITEGE,UPENDO NKONE, JANGALA SON, MWANSASU NA WENGINE WENGI WAMEREKODIA KATIKA STUDIO HIYO. WASILIANA NAO KWA NAMBA +255 656 388 404

REDIO USHINDI FM KIPENZI CHA WATU WENGI NYANDA ZA JUU KUSINI

BAHATI BUKUKU: NAFURAHIA WIMBO WA ‘WARAKA WA HAMANI’ UNAPOPIGWA BAA


Hivi karibuni blog hii ilibahatika kukutana na mkali wa muziki wa Injili nchini Bahati Bukubu na kufanikiwa kumuuliza maswali kumi yanayohusiana na huduma yake.
KTGM:Bwana Yesu asifiwa mtumishi wa Mungu Bahati
BAHATI: Amen, karibu nyumbani kwangu.
KTGM:Nashukuru. Baada ya salamu, ningependa kukuuliza swali dogo, huduma ya kuimba nyimbo za Injili kwako ni kutoka moyoni au kusaka maslahi?
BAHATI: (tabasamu) ni kutoka ndani ya moyo mpendwa.
KTGM: Nashukuru, kuna tafsiri mbalimbali kuwa, baadhi ya waimbaji kama wewe, wapo kimaslahi zaidi na ndiyo hao ambao wanachokiimba sicho wanachokifanya, ni kweli?
BAHATI: (akiwa makini) aa, sijafanya uchunguzi, maana mimi naangalia zaidi ujumbe wao kwenye muziki kuliko maisha yao binafsi.
KTGM: Watu wanasema kumtumikia Mungu kuna njia nyingi, kama hivi wewe unavyoimba, lakini je ni kweli kwamba muziki unaoimba unachangia watu kumjua Mungu?
BAHATI: (akionekana mwenye furaha) sana, naamini na nina mifano mingi ambayo kwenye blogo siwezi kuisema.
KTGM: Kuna wimbo wako mmoja unaitwa Waraka wa Hamani, wengi wameuzoa kwa jina la Ester, huu wimbo unapigwa sana kwenye baa na sehemu ambao si za kumtukuza Mungu, kwanza hilo unalijua?
BAHATI: (kicheko) najua, hilo siyo geni kwangu.
KTGM: Je, unajisikiaje kupiga muziki kwa ajili ya kumtukuza Mungu lakini watu wengine wanaufanya ni kiburudisho kwenye baa wakati wanalewa?
BAHATI: (akikaa sawa) tena nafurahi sana, maana walevi nao wanatakiwa kupelekewa ujumbe huko huko baa, kanisani na kwenye mikutanao ya wazi hawaendi, utawapata wapi kama siyo baa? Nafurahi sana. Hata Yesu aliwafuata Wayahudi kwenye Masinagogi yao.
KTGM: Unakiri kuwa, wimbo wa Waraka unaweza kuwa na chati kubwa kuliko nyimbo zako nyingine?
BAHATI: Kwangu sivyo, zote ziko kwenye chati, ila wasikilizaji wanaona kwa mtazamo wao, Waraka wameupenda sana, pengine kutokana na mpangilio wa maneno na hadithi yenyewe.
KTGM: Hapa nina swali moja la kizushi, hivi karibuni kuna mtu alijitokeza nakudai ana uhusiano wa kimapenzi na wewe, ile tuhuma ulijisikiaje?
BAHATI: (akipoteza uchangamfu) kusema kweli nilimwachia Mungu na yeye alijibu. Kwani kama utakaumbuka, uongozi wa yule kijana ambaye ni mtangazaji ulifanya uchunguzi na kubaini madai yake hayakuwa na ukweli wowote.
KTGM: Sawa, lakini tuhuma kama ile huoni kama ilikuweka pabaya, ulifanyaje kwa Mungu wako?
BAHATI: (kicheko) nilimwambia Mungu amshughulikie, naye akafanya. Unajua nimewahi kusema na sasa pia nasema, siwezi kusema namtumikia Mungu halafu nikamtumikia shetani, kama ni kuamua kufanya  umalaya hakuna sababu ya kujifichaficha. Na kuna msemo unasema kama nguruwe ni haramu basi kula aliyenona, lakini si yule kijana mtangazaji, alitaka umaarufu tu.
KTGM: Ni kweli wewe na mumeo mmeaachana?
BAHATI: Si kweli, sisi Wakristo hakuna kuachana, tumetangena, katika siku aliyoipanga Mungu tutarudiana.
KTGM: Ni mwanamuziki gani wa Injili unamkubali hapa nchini?
BAHATI: Mh! Sisi waimbaji hatuna mambo ya hivyo, wote tuko sawa, nawakubali wote na wote tunapendana.
KTGM: Asante sana, tutaonana siku nyingine.
BAHATI: Nashukuru sana, karibu tena siku nyingi leo isiwe ndiyo mwisho.

JE, UNATAKA MUIMBAJI GANI WA MUZIKI WA INJILI NCHINI NIMTAFUTE NA NIKUPE HABARI ZAKE? TUMA UJUMBE WAKO SASA KUPITIA BLOG HII PENDWA.    

Newer Post Older Post