30 wauwawa na bomu la kujitoa muhanga.
Karachi.
Mshambuliaji wa kujitoa muhanga ameshambulia mlolongo wa Waislamu wa madhehebu ya Kishia katika mji mkubwa nchini Pakistan wa Karachi na kuuwa watu 30. Kiasi watu 60 pia wamejeruhiwa. Watu walioshuhudia wamesema kuwa watu wawili ama watatu waliingia katika kundi la watu wapatao 50,000 waliokuwa wakishiriki katika maandamano ya Ashura na kulipua bomu lililokuwa limefungiwa mwilini. Mlipuko huo baadaye ulizusha ghasia mjini Karachi, mji wa kibiashara, ambapo watu wenye hasira walifanya ghasia. Lilikuwa ni shambulio la tatu dhidi ya sherehe hizo za Ashura nchini Pakistan mwaka huu. Siku ya Jumapili mshambuliaji wa kujitoa muhanga alishambulia msikiti wa Washia katika eneo linalomilikiwa na Pakistan la Kashmir na kuuwa watu saba. Bomu liliwajeruhi watu 17 mjini Karachi siku hiyo hiyo. Washia ni kiasi cha asilimia 20 ya jumla ya watu nchini Pakistan ambapo Wasunni ni wengi zaidi miongoni mwa watu milioni 167 nchini humo.
Post a Comment