Muingereza kunyongwa China
Beijing.
Muda unakaribia kufikia mwisho kwa mtu mmoja raia wa Uingereza anayekabiliwa na hukumu ya kunyongwa nchini China. Akmal Shaikh mwenye umri wa miaka 53 alikamatwa Septemba 2007 mjini Urumqi magharibi mwa China akiwa na kilo nne za madawa ya kulevywa katika mzigo wake. Alihukumiwa kifo mwaka jana , Shaikh ameshindwa katika rufaa yake ya mwisho katika mahakama kuu mwezi huu. Waungaji wake mkono wanadai kuwa baba huyo mwenye watoto watatu ni mgonjwa wa akili, utetezi ambao hauna uzito wa kutosha kwa mujibu wa sheria za China. Hukumu ya kifo inatolewa kwa makosa kadha nchini humo na hutekelezwa mara zote. Mwaka jana kiasi cha zaidi ya watu 1,700 wamenyongwa.
Post a Comment