Askofu wa Zambia avuliwa uaskofu
Aliyekuwa kiongozi wa kanisa Katoliki nchini Zambia, Askofu Mkuu Emmanuel Milingo, 79, amenyang'anywa mamlaka ya uaskofu na Vatican.
Alitengwa mwaka 2006 kwa kuoa na kujaribu kuwatawaza mapadri wanne na kuwa maaskofu.
Kanisa hilo limesema inabidi kuchukua hatua za ziada kutokana na uamuzi wake wa kuwatawaza baadhi ya mapadri mwezi Julai, jambo ambalo hufanywa na Papa peke yake.
Paul Samasumo, msemaji wa kanisa Katoliki la Zambia ameiambia BBC, "Amevuliwa wadhifa wa uaskofu na anaitwa Bw Milingo."
Mwaka 2001, Bw Milingo alimwoa mtaalamu wa kupiga chuku yaani 'acupuncturist' ambaye ni raia wa Korea ya Kusini mjini New York, Marekani.
Post a Comment