EU yaitaka Israel kuangalia upya mradi wa nyumba.
Brussels.
Umoja wa Ulaya na Marekani zimepinga mipango ya Israel ya kujenga nyumba 700 katika eneo la Jerusalem ya mashariki. Katika taarifa, umoja wa Ulaya umeutaja ujenzi wa nyumba hizo kuwa ni kinyume na sheria chini ya sheria za kimataifa, wakati msemaji wa ikulu ya Marekani Robert Gibbs ameieleza mipango hiyo kuwa ni kitisho kwa amani ya eneo hilo. Wapalestina wanataka kulifanya eneo la Jerusalem ya mashariki kuwa mji wao mkuu wa taifa wanaloahidiwa na wanaungwa mkono na jumuiya ya kimataifa pamoja na umoja wa Ulaya. Israel wakati huo huo imesema mji wote wa Jerusalem ni mali ya taifa la Kiyahudi na imekataa miito ya kusitisha ujenzi wa makaazi katika eneo la mashariki inalolikalia.
Post a Comment