Westerwelle asema Ujerumani itasusia mkutano wa Afghanistan.
Berlin.
Waziri wa mambo ya kigeni wa Ujerumani Guido Westerwelle, amesema kuwa atasusia mkutano wa kimataifa kuhusu Afghanistan, iwapo mkutano huo hautaangalia juhudi za ujenzi wa kiraia. Westerwelle ameliambia gazeti la kila wiki nchini Ujerumani la Stern kuwa iwapo mkutano huo utakaofanyika mwezi Januari mjini London utakuwa tu kuhusu kuchangia majeshi zaidi kwa ajili ya Afghanistan, Ujerumani haitashiriki. Hata hivyo, Westerwelle amerudia maelezo rasmi ya serikali kuwa itaangalia juu ya kuchangia waalimu zaidi kwa ajili ya jeshi la polisi . Kuongeza idadi ya wanajeshi wa Ujerumani nchini Afghanistan litakuwa si jambo linaloungwa mkono nchini humo.
Post a Comment