Kilaini awaanga wakazi wa Dar
Aliyekuwa askofu Mkuu Msaidizi wa Jimbo Kuu la Kanisa Katoliki la Dar es Salaam, Methodius Kilaini, ambaye amehamishiwa Jimbo la Bukoba, amewaaga rasmi waumini wa Jimbo hilo na kudai kuwa atawakumbuka kwa upendo wao waliokuwa nao juu yake(Picha kwa hisani ya Habari Leo).
Akiwaaga waumini hao kupitia ibada ya Misa ya sikukuu ya Krismasi iliyofanyika kwenye Kanisa la Mtakatifu Joseph, Kilaini alisema kuwa, mbali na kuwakumbuka, pia amewataka Watanzania wote kuliombea taifa lao ili uchaguzi mkuu wa mwakani uwe wa amani na utulivu.
Kilaini alisema kuwa, Watanzania wana wajibu wa kuwaombea viongozi wa vyama vya siasa ili washiriki katika uchaguzi huo bila kuvunja amani.
“Kama tunavyojua, mwaka kesho tuna uchaguzi, katika nchi yoyote uchaguzi ni kitu cha muhimu, tumwombe Mwenyezi Mungu uchaguzi uwe wa amani , tuwaombee wenyeviti wa vyama vya siasa ili watupitishe mwaka ujao salama na tupate viongozi watakaotufikisha miaka mitano ijayo salama,” alisema Kilaini.
Katika hatua nyingine Kilaini alitumia nafasi hiyo kuwasamehe watu wote mabaya waliyomfanyia wakati akiwa Askofu Msaidizi wa jimbo kwani ni hali ya kibinadamu na hivyo hana budi kuyasahau na pia waumini wa kanisa hilo walitumia misa hiyo kumuaga rasmi.

Post a Comment