Maaskofu wa Ireland wajiuzulu kutokana na kashfa ya ulawiti.
DUBLIN
Maaskofu wengine wawili wa kanisa Katoliki nchini Ireland wamesema kwamba watajiuzulu kufuatia kufichuka kwa kashfa kwamba dayosisi kuu ya Dublin imekuwa ikificha vitendo vya kulawiti vilivyokuwa vinafanywa na makasisi dhidi ya watoto. Maaskofu wasaidizi, Eamonn Walsh na Ray Field, wamesema wanatumai hatua yao ya kujiuzulu inaweza kusaidia kuleta amani na maridhiano ya Yesu Kristo kwa wahanga na watoto walionusirika na vitendo hivyo vya ulawiti. Ripoti iliyotayarishwa na serikali ya Ireland, imefichukua kuwa kanisa Katoliki limekuwa likificha vitendo hivyo vya kuwalawiti watoto wadogo kuanzia mwaka 1974 hadi mwaka 2004 pamoja na kuwalinda makasisi 170 waliokuwa wakiendesha vitendo hivyo wasichukuliwe hatua za kisheria.Tangu kutolewa kwa ripoti hiyo takriban mwezi mmoja uliopita, maaskofu wengine wawili, tayari wamejiuzulu.
Post a Comment