Misr yaruhusu wanaharakati 85 kuingia Gaza.
Cairo.
Serikali ya Misr jana Jumatano imewaruhusu wanaharakati 85 wa kimataifa kuingia katika ukanda wa Gaza baada ya kuomba kwa muda mrefu kuruhusiwa kuingia katika eneo hilo kupitia katika kivuko cha mpakani nchini Misr cha Rafah kwa ajili ya ujumbe wa kiutu. Hata hivyo haijafahamika iwapo wanaharakati hao, ambao wanasemekana kufikia kiasi cha 1,300 wanakubali kuruhusiwa kwa baadhi yao kuingia katika ukanda wa Gaza. Wengi wao wamekuwa wakifanya maandamano mjini Cairo kuhusiana na uamuzi wa Misr wa kuwazuwia kuingia katika ukanda wa Gaza.
Watayarishaji wa maandamano ya uhuru wa Gaza wamesema kuwa wanaharakati hao kutoka nchi 42 duniani wameingia nchini Misr kujaribu kuingia katika ukanda wa Gaza kutoa msaada na kushiriki katika maandamano ya amani wakipinga kufungwa kwa mipaka ya ukanda wa Gaza.
Post a Comment