Viongozi wa upinzani wakimbia Iran.
Shirika la habari la taifa nchini Iran IRNA, limeripoti kuwa viongozi wawili maarufu wa upinzani nchini humo wamekimbia kutoka mji mkuu Tehran kwa hofu na wamekimbilia katika jimbo la kaskazini mwa nchi hiyo. Ripoti hizo zinamaana kuwa viongozi hao wawili ni viongozi wakuu wa upinzani nchini humo , Mir Hossein Mousavi na Mehdi Karroubi. Hata hivyo , mmoja wa watoto wa Karoubi , ameliambia shirika la habari la Parleman ambalo huchukua msimamo wa kati kuwa baba yake na Mousavi wote bado wako mjini Tehran. Mamia kwa maelfu ya watu walishiriki katika maandamano kadha ya kuiunga mkono serikali, yaliyotayarishwa na viongozi wa kidini na kisiasa kutokana na wimbi la maandamano ya wapinzani ambayo yamekuwa yakifanyika nchini kote. Ujerumani na umoja wa mataifa zimewataka maafisa wa Iran kuwa watulivu wakati wakiwashughulikia waandamanaji wa wanaopinga serikali.
Post a Comment