Watu 33 wameuawa katika mapambano nchini Nigeria
Abuja:
Kumetokea mapigano makali kati ya vikosi vya usalama vya Nigeria na waumini wa dini ya kiislamu wenye imani kali ambayo yamesababisha vifo vya watu 38 katika jimbo la Bauchi.
Mkuu wa jeshi la polisi nchini humo, Atiku Kafur, ameliambia gazeti moja la nchini humo kwamba, mapigano hayo yalianza baada ya kiongozi wa dhehebu la Kalo Kato, Malam Badamasi, kukasirishwa na tetesi kwamba mmoja wa wafuasi wake alikuwa akifanya vitendo vya kishirikina dhidi yake.
Katika kujibu tetesi hizo, kiongozi huyo alianzisha mahubiri ya hadhara ambayo yaliwaudhi baadhi ya watu na hivyo kuzusha machafuko.
Wakati huo huo, polisi ya nchi hiyo inatarajia kuwa na mkutano na vyombo vya habari juu ya uchunguzi wa kesi ya Umar Farouk Abdul Muttallib, ambaye alifanya jaribio la kuiripua ndege ya abiria iliyokuwa inaelekea Detroit, Marekani, wakati wa sikukuu ya Krismas.
Post a Comment