Viwanja vya ndege vyaongeza ulinzi.
Katika mkutano na waandishi habari uliofanyika Hawaii, rais wa Marekani Barack Obama amekiri kuwa usalama wa ndani nchini humo pamoja na ulinzi kupitia taarifa za siri umepata pigo kabla ya kutokea jaribio lililoshindwa la kigaidi wakati wa sikukuu ya Chrismass.
Wakati huo huo , viwanja vya ndege nchini Ujerumani vimeongeza usalama, na kuanzisha upekuzi mkali wa wasafiri na mizigo kufuatia hatua kama hizo zilizochukuliwa na maafisa wa viwanja vya ndege barani Ulaya na Marekani. Maafisa wamewaomba wasafiri kuwa na uvumilivu kutokana na hatua hizo mpya. Kundi la kimkoa la kigaidi la al Qaeda limedai kuhusika na shambulio hilo lililoshindwa la kigaidi, likisema limempatia kijana huyo mwenye umri wa miaka 23 raia wa Nigeria kifaa hicho cha mlipuko. Matatizo ya kiufundi yalizuwia kifaa hicho kulipuka ndani ya ndege ya shirika la ndege la Northwest, ambayo ilikuwa imewachukua abiria 278 na hakuna mtu mwingine mbali ya kijana huyo aliyejeruhiwa.
Post a Comment