Serikali ya Ujerumani yaishutumu Iran .
Berlin.
Serikali ya Ujerumani imesema kuwa ina wasi wasi mkubwa kuhusu matukio ya hivi karibuni nchini Iran, na imeshutumu vikali vitendo vya majeshi ya usalama ya Iran . Naibu waziri wa mambo ya kigeni wa Ujerumani Werner Hoyer pia ameitolea wito Iran kuzuwia kuongezeka zaidi kwa hali ya wasi wasi. Katika muda wa siku za hivi karibuni kumekuwa na maandamano makubwa dhidi ya utawala wa Iran, wakati watu karibu wanane wameuwawa katika maandamano siku ya Jumapili. Miongoni mwa wale waliouwawa ni pamoja na mpwa wa kiongozi wa upinzani Mir Hossein Muossavi. Siku ya Jumanne rais wa Iran Mahmoud Ahmedinejad amelaumu kile alichosema ni Marekani na Wayahudi kwa hali hiyo ya kukosa utulivu.
Post a Comment