Clinton aonya udhaifu wa Yemen waweza hatarisha kanda nzima.
Washngton:
Waziri wa Mambo ya Nchi za nje wa Marekani Hilary Clinton ameonya kwamba udhaifu uliopo nchini Yemen, unaweza kutishia udhabiti wa eneo hilo.
Taarifa za uwezekano wa kufanyika kwa mashambulio, iliyotolewa na kikundi kinachojiita Al Qaeda katika rasi ya Arabuni, imeifanya Marekani kufunga ubalozi wake, katika mji mkuu wa nchi hiyo Sanaa, siku ya Jumapili.
Muda mfupi tu, baadaye Uingereza na Ufaransa nazo zikafanya hivyo.
Seneta wa Marekani Joseph Lieberman amesema nchi yake na Uingereza zimekuwa zikiimarisha juhudi zao za kukabiliana na ugaidi nchini Yemen.
''..Anasema wamechukua hatua katika operesheni zao kuiunga mkono serikali ya Yemen dhidi ya magaidi nchini humo, na kwamba inabidi kufanya hivyo vinginevyo Yemen itakuwa kama Iraq na Afghanistan, na kwamba hawataki hilo litokee.
Wakati huohuo, Mahakama ya rufaa nchini Marekani imethibitisha hukumu ya kifungo cha maisha kwa mshtakiwa Zacarias Moussaoui.
Mshtakiwa huyo raia wa Ufaransa, ndiye pekee aliyetiwa hatiani katika mahakama ya Marekani kwa makosa ya kuhusika katika shambulio lililotokea Septemba 11, mwaka 2001.
Moussaoui jana alishindwa jaribio la kutengua makosa yake ya kula njama katika shambulio hilo, na kuhukumiwa upya.
Post a Comment