Marekani yachunguza kwa kina washukiwa wake wa ugaidi.
Marekani inachunguza kwa kina, orodha yake ya washukiwa wa ugaidi, huku ikiwaongeza zaidi washukiwa hao katika orodha ya wale wasiotakiwa kusafiri nchini humo.
Sheria mpya katika viwanja vya ndege vya kimataifa nayo pia imeanza kutumika nchini humo, ambapo abiria wote wanaosafiri na ndege za nchi hiyo sasa wanapaswa kufanyiwa ukaguzi wa kina na mizigo yao pia kukaguliwa, na ikibidi kwa kutumia vifaa maalum vya kubaini miripuko au kumulikwa mwili mzima kabla ya kupanda ndege.
Hatua nyingine zilizoimarishwa za usalama ni kwa wasafiri wote kutoka ama kupitia nchi 14, zinazodaiwa na Marekani kuwa na uhusiano na magaidi, wanalazimika kukaguliwa kwa kutumia mashine ya kumulika mwili mzima.
Sheria hiyo mpya inafuatia jaribio lililofanywa wakati wa Krismas la kulipua ndege ya Marekani, ambalo linadaiwa kufanywa na kijana wa Kinigeria, ambaye Marekani inaamini kuwa amepewa mafunzo na mtandao wa Al Qaeda nchini
Post a Comment