Iran yaanza kujadiliwa
Washngton:
Marekani na nchi rafiki zake kidiplomasia, zimeanza kujadili vikwazo vipya dhidi ya Iran.
Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje wa Marekani Hilary Clinton, amesema madhumuni ya hatua hiyo ni kuishinikiza serikali ya Iran, bila ya kuweka ugumu wa maisha kwa wananchi wa kawaida wa Iran.
Wakati huohuo, ziara iliyokuwa imepangwa na ujumbe wa wabunge wa Umoja wa Ulaya kuitembelea Iran, imezuiwa na serikali ya nchi hiyo, bila ya kutarajiwa.
Shirika la Habari la Iran, limesema ziara hiyo imeahirishwa na Wizara ya Mambo ya Nchi za Nje ya nchi hiyo ili kupisha muda zaidi, wa kujiandaa na ziara hiyo.
Lakini hata hivyo, kiongozi wa ujumbe huo Barbara Lochbihler, amesema ziara hiyo iliahirishwa baada ya hatua ya Iran kuzuia mkutano uliopangwa kufanyika kati ya Wabunge wa Umoja wa Ulaya na viongozi wa upinzani wa nchi hiyo.
Post a Comment