MAGOKE: Ufisadi umeingia kwa watangazaji wa radio,Tv za dini
Leo nimefanikiwa kukutana na ndugu yangu Magoke Junio, wakazi wa mkoa wa Shinyanga kumuita Alpha Magoke kutokana na jina hilo kulitumia wakati akiwa shuleni hasa shule ya mzisingi.
Muimbaji huyu kwa namna moja ama nyingine ameoneka kukerwa na kile alichokiita ufisadi kwa baadhi ya watangazaji wa radio na Tv za dini, kutokana na kucheza nyimbo za watu wenye majina makubwa kwa lengo la kujipatia kipato kutoka kwa wahusika.
Magoke ambaye ni mzaliwa wa mkoa wa Shinyanga alisema kuwa, leo hii ukifika studio za vyambo hivyo vya habari utakuta CD nyingi za waimbaji zimewekwa kabatini pasipo kuchezwa huku ukisiliza nyimbo za waimbaji waliotofa fedha zikichezwa kila kukicha tena zikipambwa kwa sifa ambazo wakati mwingine mhusika anakuwa hana.
“Ninakila sababu za kusema kuwa, ufisadi umeingia kwa watangazaji wa radio,Tv za dini kw sababu leo hii ukipeleka kazi yako studio unatakiwa ulipie kwanza shilingi laki 3 ama zaidi ili kazi yako ipigwe mara kwa mara, na usipofanya hivyo, Cd yako inazikwa”.
“Ninaushahidi wa kutosha juu ya jambo hili, si kwamba waimbaji wenye majina tulionao sasa ni hao tu, bali kunawengine nyimbo zao ni kali kuliko hizo zinazosikika zenye ujumbe mzito lakini kwa kuwa wao hawana pesa ya kuwapa watangazaji hao, ndiyo maana hawasikiki”.
Magoke aliendelea kusema kuwa, wakati mwingine baadhi ya waimbaji walioinuliwa huwa wanakampeni ya kuwachombeza watangazaji hao kutopiga nyimbo za waimbaji hasa ambao huonekana kuwa tishio pindi wanaposimama nao jukwaani kutokana na jumbe zao kuwa nzuri na zenye upako wa ajabu.
Alitoa mfano mmoja kuwa, katikati ya mwaka jana, kuna tamasha la uimbaji liliandaliwa mkoani Mwanza ambalo liliwashirikisha baadhi ya wakali wa muziki wa Injili kutoka jijini Dar es Salaam, wakati wa kuimba walitangulia wakongwe ndipo akapanda jukwaani mwanadada naye kutoka Dar ambaye jina lake siku kubwa sana, alionekana kuvuta hisia za watu waliohudhuria tamasha hilo.
“Kuna tamasha la waimbaji lilifanyika mkoani Mwanza katikati ya mwaka jana, waimbaji wakonge walipewa nafasi za kwanza kuimba na watu waliwashangili kutokana na kuwafahamu majina yao, lakini alisimama mwanadada mmoja na kuimba wimbo uliovuta hisia kali kwa mashabiki wa muziki huo, na alijikuta anatunza fedha nyingi kuliko wakongwe,” alisema Magoke.
Kitendo hicho kinadhihirisha kwamba ni kweli kuna waimbaji ambao wanagandamizwa na watangazaji wa vituo hivyo, lakini wakipewa nafasi wanaweza kufanya maajabu na kuponya mioyo ya watu ambao inahitaji kuhubiriwa kwa njia ya uimbaji.
Magoke amewataka watangazaji wanaojishughulisha na vitendo hivyo kuacha mara moja, kitendo cha kukaa kwenye studio hizo ni sawa na kuwa madhabahuni, hivyo suala la kukubali kupokea hongo kama kichocheo cha kupiga nyimbo linahitaji kuachwa ili kuponya roho zao.
“Nawasihi kuachana na tabia hiyo, kwani uwepo wao katika studio hizo ni sawa na kwamba wapo madhabahuni, hivyo kuchanga masuala ya kuchukua rushwa ili wacheze nyimbo za waimbaji wachanga waache ili kuokoa roho zao, suala la muimbaji kuwapa asante ya kucheza kazi yao linaweza kutolewa na wahusika bila kujenga mazingira ya rushwa,” alisema Magoke.
Jitihada za kuwapata baadi ya watangazaji wa radio na Tv za dini zinaendela, endalea kuwa nami katika safu hii.
Mtumishi huyo wa Mungu tayari anayo albamu yake moja yenye vibao tisa ambavyo ni Mwamba uliobeba jina la albamu, Rudi, Mungu nakushukuru, Hubiri, Niko kwako, Tafuteni, Faster faster, Kanisa na Mama.
Nyimbo za Makonge zipo katika miondoko mchanganyiko, kama vile miondoko ya muziki wa kizazi kipya kwa lengo la kuwapata vijana wengi, zuku na mingine mengi.
Post a Comment