Midnight Crew' kubariki Amani ya Rwanda
Kigali, Rwanda
Kundi namba moja la muziki wa Injili duniani lenye maskani yake Kaduna nchini Nigeria, Midnight Crew, linatarajiwa kutua nchini Rwanda kwa ajili ya tamasha la kumshukuru Mungu kutokana na kuleta amani nchini hapa iliyokuwa imepotea kwa muda mrefu linalotarajiwa kufanyika mapema mwezi ujao.
Midnight Crew wataungana na kundi lingine linaloshikilia namba mbili kwa ubora wa makundi ya muziki huo dunia kwenye uwanja wa Amahoro na wataungana na waimbaji wengine kutoka kila mikoa ya hapa.
Akizungumza kwa niaba ya wanamuziki wenzake kiongozi wa kundi hilo, Gbenga Oyebola alisema kuwa, mwaliko wa kuja kuimba nchini hapa umetolewa na serikali ya Rwanda na wanauhakika watafanya kazi ya Mungu vizuri ili taifa hili liendelee kubaki na amani iliyopo hivi sasa.
Waimbaji wengine wanaounda kundi hilo ni Patricia-Uwaje King, Odunayo Ojo na Michael Abdul
Post a Comment