LULU, PACHA WA DOTNATA NDANI YA MBEYA AGOSTI 4,2013

WASANII WA FILAMU NCHINI ELIZABETH MICHAEL (LULU) NA PACHA WA DOTNA NI MIONGONI MWA WAGENI WATAKAOHUDHURIA TAMASHA LA KUITAMBULIA ALBAM YA NITANG’ARA TU YA MWINJILISTI KABULA GEORGE UTAKAOFANYIKA KATIKA MKOA WA MBEYA TAREHE 4 MWEZI WA 8, 2013. SEHEMU AMBAPO LITAFANYIKA TAMASHA HILO ITATANGAZWA HIVI KARIBUNI. WASILIANA NASI KWA SIMU NAMBA 0755 240136/0712001880.

JIPATIE SOFA SAFI KWA KOMBA SOFA SHOORM MKOANI MBEYA

KOMBA SOFA SHOORM (YESU NDIYE) NI WATENGENEZAJI WA SOFA ZA KISASA NA KUZIUZA KWA GHARA NAFUU SANA. WAPO MBEYA STRIRED JIRANI NA KANISA LA HIJA MWANJELWA JIRANI NA KANISA KUBWA WA ROMA. WASILIANA NAO KWA SIMU NAMBA 0754553467 AU 0655 553467. NYOTE MNAKARIBISHWA.

ECK PRODUCTION STUDIO YA KISASA NA KIMBILIO LA WAIMBAJI WA MUZIKI WA INJILI TANZANIA.



IPO MWEMBECHAI JIJINI DAR ES SALAAM, TANZANIA WAIMBAJI KAMA ROSE MUHANDO, HABATI BUKUKU, BONY MWAITEGE,UPENDO NKONE, JANGALA SON, MWANSASU NA WENGINE WENGI WAMEREKODIA KATIKA STUDIO HIYO. WASILIANA NAO KWA NAMBA +255 656 388 404

REDIO USHINDI FM KIPENZI CHA WATU WENGI NYANDA ZA JUU KUSINI

Mtikila aachiwa kwa dhamana

HATIMAYE Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam, imemuachia huru Mwenyekiti wa Chama Cha Demokratic (DP), mchungaji Christopher Mtikila, baada ya kukamilisha masharti ya dhamana katika kesi ya tuhuma za kupuuza kuhudhuria mahakamani.

Mchungaji huyo amekuwa mahabusu kwa zaidi ya wiki mbili zilizopita, kufuatia agizo la mahakama la kutaka akamatwe kwa kushindwa kuhudhuria kesi yake, inayohusu tuhuma za kumkashifu Rais Jakaya Kikwete.
Mapema wiki hii, wakili wake aliiomba mahakama impatie dhamana mteja wake.
Uamuzi wa mahakama kukubali ombi hilo, ulifikiwa jana na Hakimu Mkazi, Waliarwande Lema, baada ya kiongozi huyo wa DP, kukamilisha masharti ya kuwa na wadhamini wawili ambao kila mmoja,alisaini bondi ya Sh1 milioni.
Pamoja na kutimiza masharti hayo, mchungaji Mtikila pia ametakiwa kusalimisha mahakamani, hati yake ya kusafiria na asitoke nje ya Jiji la Dar es Salaam, bila kibali.
Februari 8, mwaka huu atasomewa maelezo ya awali kuhusu kesi inayomkabili, hatua inayokuja baada ya upande wa mashtaka kukamilisha upelelezi.
Januari 21, mwaka huu mchungaji Mtikila, kupitia wakili wake Mpale Mpoki, aliwasilisha ombi kwa mahakama kuiomba itengue uamuzi wa kumfutia dhamana.
Hata hivyo wakili wa serikali, Ponsiano Lukosi alilipinga ombi hilo kwa madai kuwa Mahakama ya Kisutu, haina uwezo wa kutengua uamuzi ambao ulikwishautoa.
Lukosi aliiambia mahakama hiyo kuwa kama upande wa utetezi unataka dhamana hiyo itenguliwe, basi inapaswa kwenda Mahakama Kuu ya Tanzania.
Akimfutia Mtikila katika kesi ya kashfa dhidi ya Rais Kikwete, hakimu Lema alisema mahakama imefikia uamuzi huyo kwa sababu hakuna sababu za msingi zilizokuwa zimetolewa na Mtikila juu ya kushindwa kuhudhuria mahakama.

HABARI HII NI KWA MJIBU WA GAZETI LA MWANANCHI

Newer Post Older Post