LULU, PACHA WA DOTNATA NDANI YA MBEYA AGOSTI 4,2013

WASANII WA FILAMU NCHINI ELIZABETH MICHAEL (LULU) NA PACHA WA DOTNA NI MIONGONI MWA WAGENI WATAKAOHUDHURIA TAMASHA LA KUITAMBULIA ALBAM YA NITANG’ARA TU YA MWINJILISTI KABULA GEORGE UTAKAOFANYIKA KATIKA MKOA WA MBEYA TAREHE 4 MWEZI WA 8, 2013. SEHEMU AMBAPO LITAFANYIKA TAMASHA HILO ITATANGAZWA HIVI KARIBUNI. WASILIANA NASI KWA SIMU NAMBA 0755 240136/0712001880.

JIPATIE SOFA SAFI KWA KOMBA SOFA SHOORM MKOANI MBEYA

KOMBA SOFA SHOORM (YESU NDIYE) NI WATENGENEZAJI WA SOFA ZA KISASA NA KUZIUZA KWA GHARA NAFUU SANA. WAPO MBEYA STRIRED JIRANI NA KANISA LA HIJA MWANJELWA JIRANI NA KANISA KUBWA WA ROMA. WASILIANA NAO KWA SIMU NAMBA 0754553467 AU 0655 553467. NYOTE MNAKARIBISHWA.

ECK PRODUCTION STUDIO YA KISASA NA KIMBILIO LA WAIMBAJI WA MUZIKI WA INJILI TANZANIA.



IPO MWEMBECHAI JIJINI DAR ES SALAAM, TANZANIA WAIMBAJI KAMA ROSE MUHANDO, HABATI BUKUKU, BONY MWAITEGE,UPENDO NKONE, JANGALA SON, MWANSASU NA WENGINE WENGI WAMEREKODIA KATIKA STUDIO HIYO. WASILIANA NAO KWA NAMBA +255 656 388 404

REDIO USHINDI FM KIPENZI CHA WATU WENGI NYANDA ZA JUU KUSINI

Polisi wawatia hofu waumini wa Kakobe

Leon Bahati
KIKOSI cha askari polisi wapatao 10, kimezusha hali ya wasi wasi katika maeneo ya Mwenge, jijini Dar es Salaam baada ya kujipangakatika eneo la karibu na Kanisa la Full Gospel Fellowship, ambalo wiki tano zilizopita, askofu wake, Zachary Kakobe alilitangaza kuwa la hatari kwa wafanyakazi wa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco).
Askofu Kakobe alitangaza hali hiyo baada ya Tanesco kutoa tamko la kutaka kupitisha njia ya umeme ya msongo mkubwa, mbele ya kanisa hilo licha ya waumini wake kupinga hatua hiyo kwa madai kuwa itaathiri mitambo ya kurekodi ibaada na kituo cha televisheni kinachotarajiwa kufunguliwa hivi karibuni.
Tangu wakati huo waumini wa kanisa hilo wameimarisha ulinzi nje ya kanisa hilo ili kuhakikisha kuwa mafundi wa Tanesco, hawaendelei na mpango wa kupitisha njia ya umeme ya kilovoti 132.Jana mchana baadhi ya wakazi wa Mwenge walipigwa na butwaa kuona askari wakiwemo watatu waliokuwa wamevalia sare huku wakiwa wamebeba bunduki na kujipanga umbali wa mita 10 kutoka kwenye eneo ambalo waumini wapatao 100, walikuwa wanalinda.
Waumini hao walikuwa wamevalia fulana za rangi ya njano na walikuwa wametulia katika eneo ambalo halina kivuli bila kujali jua, waliliambia Mwananchi kuwa wako tayari kupambana na askari hao.
Tukio hilo limekuja wiki mbili tu baada ya Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja kuzungumza na Askofu Kakobe kuhusu namna ya kumaliza mgogoro wa eneo hilo kwa njia ya amani.
Taarifa zililifikia gazeti hili jana zilisema askari hao walkwenda katika eneo hilo kwa lengo la kusimamia mafundi wa Kampuni ya Becco ambayo Tanesco imeipa kazi ya kutengeneza njia hiyo ya umeme.
Mafundi hao walikuwa wapime umbali uliopo kati ya Barabara ya Sam Nujoma na kanisa hilo lakini baada ya kuwasiliana na Askofu Kakobe, aliwakatalia kwa maelezo kuwa hawakumpa taarifa mapema.
Askari hao waliojipanga eneo hilo waliondoka saa saba mchana baada ya mafundi wa Kampuni ya Becco kutopata ridhaa ya askofu huyo ili kuendelea na kazi ya kupima eneo hilo.
Mwananchi lilipowasiliana na Kakobe, alisema wakati tukio hilo linatokea, alikuwa nje ya eneo la Mwenge kwa shughuli za kikanisa na alikataa kutoa ridhaa kwa sababu walipaswa kumuarifu mapema.
Alikiri kuwa kwenye mazungumzo yao na Wazairi, walikubaliana kupima umbali kati ya barabara na kanisa ili kujua athari za njia hiyo ya umeme lakini kilichomshangaza hawakutokea katika siku walizokubaliana.
Awali, Kakobe alisema kwamba Tanesco walilazimisha njia hiyo ipite upande wa barabara hiyo ambako kanisa lipo baada ya uongozi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, kuwakatalia kupitisha upande mwingine wa barabara hiyo.

Newer Post Older Post