Simu za mkono na mtandao wa internet kukaguliwa vikali zaidi nchini Iran
TEHRAN:
Mkuu wa polisi nchini Iran Ismail Ahmadi Moghaddam amesema, kutakuwepo ukaguzi mkali wa simu za mkono na mtandao wa internet nchini humo na hatua kali zitachukuliwa dhidi ya wale wanaoitisha maandamano kupitia njia hiyo. Amesema watu hao hawatoweza kujificha.
Takriban magazeti yote yanayopendelea mageuzi na hata tovuti za wapinzani wa serikali zimefungwa, tangu kuchaguliwa tena kwa Rais Mahmoud Ahmedinejad Juni iliyopita. Kwa hivyo, wanaharakati wanatuma habari fupi na barua pepe kuitisha maandamano.
Post a Comment